Mbunge wa korogwe vijijini Timotheo Mzava akerwa na kasi  ndogo ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa maji mazinde huku akitaka fundi aliopo  aondolewe  kwa kushindwa kumaliza  kwa wakati mradi huo uliogharimu zaid ya shilingi  bil.51 zilizotolewa na Serikali ya awamu ya tano

Akizungumza  wakati wa Mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi kwa kukichagua chama cha Mapinduzi CCM na yeye  kuwa Mbunge  wa jimbo hilo uliofanyika  kata ya Mazinde wilayani korogwe

Mbunge huyo  alisema mradi huo ungewasaidia wananchi kupata maji safi na salama  ulikuwa ukamilike tangu mwaka jana  mwezi wa 11 lakini hadi  Sasa haujakamilika na wananchi wanaendelea adha ya  kukosa maji ya uhakika huku wakiuziwa maji kwa sh? 2200 kwa mwezi.

Mbunge huyo alisema mradi huo unasimamiwa na Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira  vijijini (Ruwasa) kasi yake hailizishi hivyo aliwataka viongozi wa chama na Serikali kata kumuita  Meneja wa Ruwasa ili awaeleze matumizi ya hizo pesa zaid ya milion 51 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ukarabati wa mradi huo zimefanya kazi gani licha ya muda wa kukabidhi mradi huo umeshapita .

"Ruwasa ili anzishwa kisheria kwa ajili ya  kuongeza kasi  ya kupeleka maji kwa wananchi lakini chaajabu nyie mnafanya  kazi  na mafundi wenu hata Kijiji na kata  hawajui  mnafanya nini licha ya wananchi hao kutambua Serikali yao imewaletea shilingi million 51 za ukarabati wa mradi wa maji " Alisema Mbunge huyo.

 fundi aliyepewa mradi huo  Bakari Mtawazo alisema changamoto kubwa iliyofanya mradi usikamilike kwa wati ni kutokana na ardhi ya Mazinde kuwa na mawe makubwa na mwamba ambao hauchimbiki hivyo  kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi  ambapo alieleza kwa  Sasa wameshapata watalaam wanaochoma mawe ili waweze kukamilisha mradi huo hivyo mwezi mmoja tuliopewa tutakuwa tumeshakamilisha.

Alisema mradi huo wa ukarabati ulikuwa ukamilike mwezi wa 11 mwaka jana Kama mkataba ulivoonyesha lakini kulingana na sababu zilizotajwa hapo juu na ikiwemo ya ucheleweshwaji wa fedha ndio imepelekea kutufanya usikamilike kwa wakati.

Mtawazo alifafanua  mradi huo unajumla ya mita 1350  na mita ambazo zimechimbwa  na kulazwa mabomba ni mita 650 na kwamba mita ambazo ziko tayari ni 400 na mita ambazo bado 300 na hizo zimechelewa sababu kulikuwa na changamoto ya wakulima wa tangawizi ambao walikuwa hawajavuna.

Hata hivyo Mhandisi wamaji kutoka  Wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira (Ruwasa) Korogwe Joyce Malekela  alisema walipokea zaidi ya milion 127 kutoka serikalini kwaajili ya kukarabati  wa miradi tisa iliyoathiriwa na mafutiko  ikiwemo huu wa Mazinde  ambao haujakamilika kutokana  na changamoto mbalimbali.

Malekela  alisema kuwa kwasasa wamesharekebisha baadhi ya changamoto hivo wamempa mwezi mmoja fundi  anayetekeleza mradi huo akamilishe ili wananchi waweze kupata maji ya uhakika na waondokane na changamoto inayowakabiri  na tatizo la maji liwe historia.

Mzava ameanza ziara rasmi  ya kupita kuwashukuru wananchi  kwa kumchagua yeye na chama  chake  ambapo ameanza na kata ya  Mazinde Kama Mgombea urais ambaye kwasasa Ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  alivopita Mazinde wakati was kampeni alimtaka atakapo anza ziara aanzie kata hiyo ya maazinde.

Mbunge wa Korogwe vijijini Timotheo Mzava

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...