*Atekeleza Kampeni ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani, azindua visima sita

*Uchimbaji na Ujenzi wa Visima Vingine 20 Unaendelea

Na Mwandishi Wetu, Bariadi

NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Andrea Mathew ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi, leo amezindua visima 6 vya maji kwenye Kata tatu za jimbo hilo ikiwemo kata ya Ihusi, Nkololo na Mwaumatondo ambapo kila kata imepata visima viwili.

Ujenzi wa visima hivyo ni mwendelezo wa kampeni ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya Kumtua Mama Ndoo Kichwani ili kuongeza upatikanaji wa maji karibu na makazi ya wananchi na kupunguza adha kwa wanawake ya kutumia muda mwingi kutafuta maji ili kuwapa wananchi fursa ya kufanya majukumu mengine katika jamii zao ili kujiongezea kipato.

Uzinduzi huo umefanyika kwenye kijiji cha Bubale kilichopo Kata ya Nkololo ambapo amemtweka ndoo ya maji kichwani Nkwimba Maduhu, mmoja wa wakazi wa kijiji hicho wa niaba ya wanawake wengine na wananchi waishio kijijini hapo.

Mhandisi Kundo ameongeza kuwa uchimbaji na ujenzi wa visima vingine 20 unaendelea kwenye Kata ya Dutwa na Ngulyati na atavindua mara baada ya kukamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...