Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
WANANCHI wa eneo la Kitunda Mtaa wa
Bunju B, Kata ya Mabwepande,
Kinondoni, Jijini Dar es Salaam,
wameiomba serikali kuwasaidia baada ya kuishi kwa hofu kutokana na tishio la chatu.
Wananchi hao walitoa kilio hicho leo katika kikao kilichoitishwa na Diwani wa Kata
ya Mabwepande Mhajilina Kassim maarufu
kama Obama.
Mkutano huo
ulianza kwa wananchi hao kufanya usafi katika eneo itakapojengwa Shule ya Msingi Bunju B ambapo walifyeka eneo hilo ili kuanza ujenzi.
Pia wakiongozwa na diwani huyo walifanya msako wa chatu kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi.
Walisema licha ya chatu pia
kwenye eneo hilo wameonekana
wanyama wakali kama vile chui na mamba.
Akizungumza
na wananchi hao, Diwani Kassim
alisema anamini serikali ni
sikivu itawasaidia kukabiliana na tishio la chatu hao wanaodaiwa kuzagaa
mtaani.
Obama
aliszema chanzo cha kuzaliana kwa chatu na wanyama wakali katika eneo
hilo ni kuwepo kwa pori ambalo lina mgogoro kwa miaka zaidi ya saba.
Alisema
pori hili liko karibu na eneo ambalo shule
ya msingi itajengwa, hivyo kuiomba serikali kuingilia kati ili kesi ya mgogoro wa eneo hilo iliyopo Mahakama Kuu ya
Ardhi kumalizika.
“Hatuna
mamlaka ya kuingilia kati kesi ila tutaiandikia maombi mahakama ituruhusu
kufyeka eneo hili ili kuepusha chatu kuzaliana,”alieleza Obama.
Alisema
tayari Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni imetoa sh. milioni 156 kujenga madarasa tisa katika eneo hilo.
“Hatuna shule hapa Kitunda, shule ipo upande wa pili wa Barabara
ya Bagamoyo, Mtaa wa Kiyonzile, hivyo ujenzi wa shule hii mpya ni muhimu
ili kuepusha watoto kugongwa na magari au tishio hili la chatu na wanyama
wakali.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Bunju B, Athuman Njama ,
alithibitisha wananchi wake kuishi katika tishio la chatu hao aliodai
wanalanda mara kwa mara mtaani.
“Wananchi
wanaishi kwa hofu hapa.Wengi wanajifungia mapema ndani,”alisema Njama.
Aliongeza:
“Tunaomba serikali ije itusaidie kuwinda wanyama hawa.”
Mzee Asheli Ishiriyo, mkazi wa eneo hilo alisema hivi karibuni chatu mkubwa alikutwa akimmeza mbwa katika banda la jirani
yake.
“Alikuwa ni
mkubwa kama nguzo ya umeme. Alipo tuona alimtema mbwa na kutuvimbia ili
kukabiliana na sisi. Tukakimbia,”alieleza mzee huyo.
Ally Said,
alisema mwezi mmoja uliopita walifanikiwa
kumuua chatu mmoja na kumfukia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...