NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Abdallah Ulega akiwakabidhi zawadi ya udhamini wa masomo ( Scholership) wachezaji waliofanya vizuri kwenye ligi ya Taifa ya mpira wa kikapu ya "CRDB Bank Taifa Cup 2020" katika hafla iliyofanyika leo tarehe 18/01/2021 katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Naibu Waziri Ulega alivitaka vyama na Mashirikisho ya michezo kuwa wawazi na wawajibikaji katika matumizi ya fedha za wadhamini ili kuwapa imani wadau wengi zaidi kuwekeza na kudhamini michezo.

Aidha, ametoa rai kwa CRDB Bank kudhamini mashindano yajayo ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA ili kusaidia katika kuibua vipaji vya vijana shuleni.

Pia, Naibu Waziri Ulega ametoa wito kwa wawekezaji na makampuni mbalimbali kusaidia katika ujenzi wa miundombinu ya michezo hapa nchini kupitia fedha za Corporate Social Responsibility - CSR ili vijana wengi waweze kunufaika.

Kupitia udhamini huo, CRDB wamewapatia wanamichezo 25 takribani shilingi milioni 50 kwa ajili ya kugharamia masomo katika vyuo mbalimbali hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...