Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Klabu ya Soka ya Simba imekamilisha usajili wa aliyekuwa Mshambuliaji wa FC Platinum ya Zimbabwe, Perfect Chikwende usiku wa leo, Januari 15, 2021.
Chikwende ametajwa mara nyingi katika Mitandao ya Kijamii akihusishwa kusajili kati ya Simba SC na Azam FC, lakini Simba SC wamefanikiwa kufika makubaliano na FC Platinum kwa kumsajili Mshambuliaji huyo kwa uhamisho wa moja kwa moja (Permanent Transfer).
Chikwende anakumbukwa kuwafunga Simba SC katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Hatua za awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).
Kupitia Mitandao yake ya Kijamii, Simba SC imesema kwa majigambo. “Tunasajili kwa ajili ya malengo makubwa ya Klabu hii kubwa na hiyo ndio maana ya NEXT LEVEL”, wamesema Simba SC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...