Na Prisca Ulomi, WMTH
 
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali itaweka mazingira wezeshi ya kuendeleza vijana wabunifu wa TEHAMA nchini
 
Ndkt. Ndugulile ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (COICT) zilizopo Dar es Salaam
 
Amesema kuwa vijana wanabuni mifumo mbali mbali ya TEHAMA ya kutatua changamoto za wananchi ila wanakosa mazingira wezeshi ya kuendeleza na kukuza bunifu zao kama vile kupatiwa muda maalumu wa kuingiza sokoni bunifu zao kwa kufanya majaribio ya bunifu hizo kukubalika kwa wananchi bila kulazimika kulipia gharama za usajili, kupata masoko, malipo ya kodi na leseni kuendana na matakwa ya uendeshaji wa kampuni na biashara nchini
 
Amesisitiza kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza wabunifu wa TEHAMA ili waweze kutengeneza mifumo kuendana na mahitaji ya wananchi badala ya kuendelea kununua mifumo hiyo kwa gharama kubwa kutoka nje ya nchi ambapo Serikali inatumia fedha nyingi kununua mifumo ya TEHAMA
 
Amefafanua kuwa utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA hapa nchini utaongeza wigo wa matumizi ya intaneti na huduma za mawasiliano na itajibu changamoto za wananchi na ametoa rai kwa watanzania kujenga imani ya kutumia teknolojia rahisi zinazobuniwa na vijana wa ndani ya nchi bila kujali umri, uzoefu au majina ya kampuni zao
 
Naye Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema kuwa vijana haom wameanzisha kampuni zaidi ya 20 za mifumo ya TEHAMA na tayari mifumo hiyo inasaidia kukusanya kodi kwenye halmashauri; kuwawezesha vijana kusoma VETA kwa njia ya mtandao na TIGO kuweza kuhifadhi taarifa za wateja wake
 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu, utafiti na ubunifu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Benadetha Kiliani na Mkuu wa Ndaki ya TEHAMA ya Chuo hicho, Dkt. Mussa Kisaka wamesema kuwa Chuo kiko tayari kushirikiana na Wizara ili kuendeleza vijana wabunifu na watafiti wa TEHAMA nchini
 
Akizungumza kwa niaba ya vijana wabunifu wa TEHAMA, Geofrey Magila ameiomba Serikali kuwawezesha wakubalike na kuaminika na wapewe kazi badala ya kampuni zao kufanya kazi kwa kutumia mgongo na majina ya kampuni nyingine kwa kuwa kampuni zao ni changa na hazina mtaji wa kutosha kuingia kwenye ushindani wa zabuni zinazotangazwa zinazohusu mifumo ya TEHAMA
 
“Tulipata kazi kutoka kampuni ya AIS ya simu za mkononi ya Malyasia yenye wateja zaidi ya milioni 50 ambao walituamini na tuliwatengenezea mifumo ya kulinda taarifa za wateja wao, ndipo baadae baadhi ya kampuni za ndani ya nchi zikaanza kutuamini,” amesema Magila

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akipata taarifa kuhusu kampuni ya TEHAMA ya Magila Tech iliyoanzishwa na Godfrey Magila (anayezungumza) wakati wa ziara yake kwenye Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Antony Elias kuhusu mashine inayojiendesha yenyewe ya kutotolesha mayai wakati wa ziara yake kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) akimsikiliza Anorld Matemu (anayezungumza), mbunifu wa mfumo wa TEHAMA wa kupima ubora wa maji wakati wa ziara yake kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam
Mkuu wa Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Mussa Kisaka akitoa maelezo kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) kuhusu kampuni za TEHAMA zinazobuniwa na wanafunzi wa Chuo hicho wakati wa ziara yake chuoni hapo, Dar es Salaam
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza mwalimu wa vijana wabunifu wa TEHAMA, Dickson Kamala wakati wa ziara yake kwenye Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Alvina Minja kuhusu mfumo wa TEHAMA alioutengeneza wa kuwawezesha wazazi kupata taarifa za wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wakati wa ziara yake  kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar Salaam, Dar es Salaam
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa nne kulia) akimsikiliza Oscar Mashauri kuhusu vifaa vya TEHAMA vinavyotumika kutoa mafunzo ya mtandao kwa wanafunzi wakati wa ziara yake kwenye Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam

 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa kwanza kulia) akimsikiliza Saida Ally, mkufunzi wa TEHAMA kwa wasichana alipotembelea Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dar es Salaam

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu akitoa taarifa kwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) kuhusu ubunifu na utafiti katika TEHAMA wakati wa ziara ya Waziri huyo kwenye taasisi hiyo, Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni mwakilishi wa Katibu wa Wizara hiyo, Kitolina Kippa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...