Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Madaba mkoani Ruvuma Theofanes Mlelwa aliyevaa kapelo akiangalia moja  kati ya nyumba sita za wakuu wa Idara wa Halmashauri hiyo zinazojengwa na Serikali kwa ajili ya kuishi wakuu wa idara ambapo mara zitakapokamilika zitasaidia sana kupunguza changamoto ya wakuu wa idara kuishi mbali na eneo la kazi.

Picha na Muhidin Amri

………………………………………………………………….

Na Muhidin Amri,Madaba

SERIKALI imeipatia Halmashauri ya wilaya Madaba mkoani Ruvuma, kiasi cha shilingi milioni  600 kati ya hizo milioni 300 zitatumika kwa ajili ya  kujenga nyumba ya kuishi  Mkurugenzi Mtendaji  na  nyumba sita za wakuu wa idara wa Halmashauri.

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Madaba Mwandishi Nchimbi amesema,  nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji ni ghorofa 1 na zile za watumishi  ambazo gharama yake ni milioni 300 ni za kawaida  na ziko katika hatua ya lenta.

Nchi mbi alisema,  nyumba hiyo itakapokamilika itamwezesha Mkurugenzi kuwa na makazi bora karibu na ofisi, hivyo  kutekeleza majukumu yake ipasavyo pamoja  na kuondoka kuishi katika nyumba ndogo iliyojengwa kwa ajili ya mtumishi wa idara ya Afya.

Alisema, ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi na nyumba za wakuu wa Idara zinajengwa kwa kutumia  mfumo wa force akaunti ambapo Halmashauri inanunua vifaa na kuwapa mafundi, badala ya utaratibu wa zamani  kuwatumia wakandarasi ambao ulichangia  kuchelewesha ujenzi wa miradi mingi.

Kuhusu nyumba za wakuu wa idara alisema, zitaongeza morali ya watumishi kufanya kazi kwa kujituma  kwani zitamaliza  changamoto ya umbali kutoka katika makazi yao  hadi ofisi za Halmashauri, jambo lililo sababisha hata baadhi ya watumishi kuhama na kwenda kufanya kazi katika Halmashauri na meneo mengine nchini.

Hata hivyo alisema, changamoto kubwa katika Utekelezaji wa miradi hiyo inajenga kipindi cha masika kwa hiyo wanashindwa kusafirisha vifaa hadi eneo la ujenzi kutokana na magari kukwama  na madereva wanalazimika kupaki mbali na mradi na jamii inayowazunguka kutokuwa tayari kwenda kufanya kazi.

Kwa upande wake Mhandisi  anayesimamia ujenzi huo Shaban Kasanzu alisema,  kwa nyumba ya Mkurugenzi  ujenzi umefikia hatua ya kumwaga jamvi na kuhaidi kwamba jengo hilo litakuwa na ubora wa hali ya juu na litakamilika kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Madaba Shafi Mpenda alisema, ujenzi umeshaanza na unaendelea vyema  ambapo ameishukuru Serikali  kuipatia Halmashauri hiyo kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya nyumba  6 za watumishi  na nyumba 1 ya kuishi Mkurugenzi.

Alisema, kupitia  vikao mbalimbali na wakuu wa idara walikubaliana  nyumba hizo kujengwa karibu na ofisi ili kuwarahisishia wakuu wa idara watakaoishi katika nyumba hizo kuwahi kazi  na kutekeleza majukumu yao ya utumishi kwa muda muafaka.

Alisema, katika suala la usimamizi na ufuatiliaji wa  ujenzi  kila  nyumba  imekabidhiwa kwa mkuu wa idara na msaidizi  wake kwa barua ili kusimamia kwa karibu ujenzi  na kufahamu changamoto zinazowakabili  mafundi.

Alisema, jukumu  kubwa la Mkuu wa idara ni kusikia changamoto  zilizopo, kutoa maoni yake  na kufikisha kwa kamati ya  husika ya manunuzi,ujenzi na ufuatiliaji  ambazo wajumbe wake ni Mkuu wa wilaya,Mkurugenzi na Afisa Mipango kwa ajili ya kuzipatia majibu  ili kuhahakisha    nyumba hizo zinakamilika kwa wakati uliopangwa.

Alisema, nyumba hizo zitaleta tija kubwa kwa wakuu  wa idara,  na  kwa mujibu wa kanuni za Utumishi wa Umma, Serikali inatakiwa  kuwapa nyumba za kuishi  zenye staa  wakuu wa idara na kama serikali itashindwa kumpa nyumba basi inawajibu wa kumlipia kodi  katika nyumba atakayoishi.

Pia Mpenda alisema, ujenzi wa nyumba hizo utasaidia sana kuokoa fedha ambazo zingetumika kulipia kodi  nyumba na  watumishi kukaa katika eneo moja ambalo litawaletea  heshima  kubwa kwa jamii kuliko  kuchanganyika na watu wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...