Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi wa Jiji la Dar es salaam wanaohudumiwa na Mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Chini kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma ya Maji kuanzia siku ya Jumanne tarehe 05/01/2021 hadi siku ya Jumatano tarehe 06/01/2021.
Sababu: Kuruhusu usafishaji wa clarifier kazi itakayopelekea upungufu wa uzalishaji maji kwa asilimia 25 na kuathiri huduma ya maji kwa saa 24 katika maeneo yanayo hudumiwa na mtambo huo
Maeneo yatakayoathirika ni: Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa Ndege, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili na Kigamboni Navy na Ferry.
DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Wasiliana nasi huduma kwa wateja 0800110064 (Bure), 0735 212020 (Whatsap tu)
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano na jamii- DAWASA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...