Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akimkabidhi Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Taifa ( Taifa Stars) John Bocco fedha za posho za ndani za wachezaji pamoja na bonasi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DRC ikiwa ni sehemu ya mchango wa Serikali kusaidia maandalizi ya timu hiyo kuelekea mashindano ya CHAN 2021 nchini Cameroon.
Katika hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Ulega pia aliwakabidhi viongozi pamoja na wachezaji wa timu bendera ya Taifa.
"Serikali imechangia zaidi ya shilingi Milioni 60 kama bonasi na posho za ndani za wachezaji na benchi la ufundi, bado tunapambana kupata fedha ili kusaidia katika maeneo mengine, TFF hakikisheni mnasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha hizi pamoja na nidhamu kwa vijana ili timu yetu iweze kutuwakilisha vyema" alisisitiza Mhe. Ulega.
Taifa Stars imeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Cameroon kushiriki michuano ya CHAN 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...