NA Neema Mbuja, Rukwa
Shirika la umeme Tanzania TANESCO kupitia Idara ya masoko imeendelea na kampeni ya kutoa Elimu kwa wamiliki wa viwanda,machimbo ya madini, na mashine za kusaga kwa mkoa wa Rukwa ili kuwapatia Elimu juu ya matumizi Bora ya umeme sanjari na kukagua miundo mbinu ya umeme pamoja na mota zinazotumiwa kwenye kuendesha mashine viwandani
Miongoni mwa Elimu wanayopatiwa Ni pamoja na namna ya kutumia vifaa ambavyo vinatumia umeme kidogo, umuhimu wa kukagua mota zao Mara kwa Mara kwa ajili ya kuleta ufanisi na Usalama wa miundo mbinu ya TANESCO kwenye maeneo yao
Akizungumza na wamiliki wa viwanda kwenye Wilaya za Sumbawanga mjini na Laela , mhandisi kutoka kutoka idara ya utafiti Baraka Kanyika amesema kuwa kwa Sasa baadhi ya viwanda vinatambua umuhimu wa kufunga power factor ingawa baadhi bado hawajatambua
Kuhusu wamiliki wa mashine za kusaga Kijiji Cha muze Wilaya ya Laela mkoa wa Rukwa mhandisi Kanyika ameshauri kuendelea kuwapatia Elimu ya umuhimu wa kukagua mota zinazoendesha mashine zao Mara kwa Mara ili kuziongezea ufanisi wa utendaji kàzi na kulinda miundo mbinu ya shirika.
<
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...