*Mjadala Mtaala kuwaandaa waandishi waibua maswali mengi
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SERIKALI imetakiwa kuandaa mitaala ya uandishi wa habari inayoakisi soko ili kusaidia vijana wanaotoka vyuoni kufanya kazi kwa ufanisi na kuendana na hali halisi pamoja na kukabiliana na changamoto za utendaji.
Akizungumza jijini jana kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA Alinanuswe Kabungo katika ufunguzi mkutano wa pamoja wa vituo vya utangazaji,vyuo vya uandishi wa habari na taasisi zinazohusika na uandaaji wa mitaala alisema ushauri huo ulitolewa na wadau wa habari nchini wanaofanya kazi katika vyombo vya habari kupitia vikao mbalimbali walivyokaa na mamlaka hiyo.
Alisema vijana wanaoajiriwa kutoka vyuoni hata wale waliopo kwenye ajira wamekiri kutofundishwa wala kudokezwa masuala yanayohusu sheria na kanuni zinasimamia sekta ya utangazaji.
"Uandishi wa habari haiakisi hali halisi ya soko na kufanya utendaji kazi wa vijana hawa kukabiliana na changamoto nyingi za kiutendaji,"amesema Kabungo.
Amesema teknolojia ya habari na mawasiliano imebadilika kwa kasi hivyo uandaaji wa habari uchakataji wa habari na uwasilishaji wa habari kwa wananchi unabadilika.
Ameema hakuna semina,warsha,makongamano yanayoratibiwa na vyuo au wasimamizi na vyuo kujadili masuala yanayohusu maendeleo ya sekta ya habari na mabadiliko yanayotokea kwenye soko.
Kabungo amesema TCRA ina jukumu la kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ufanisi mkubwa kwenye sekta ya utangazaji katika wanajenga nyumba moja.
Naye muhadhili wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) Dotto Bulembu alisema mitaala ya vyuo inaandaliwa na serikali hivyo ni vizuri serikali inapaswa kushirikisha wadau ili kujua mahitaji ya wanataaluma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...