Kaimu Meneja wa Mamlaka ya  Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Sophia Mziray akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani ) kuhusiana na mikakati mbalimbali waliojiwekea katika kufanya udhibiti Dawa na Vifaa Tiba, jijini Mwanza.


*Yawaasa wafanyabiashara kufuata taratibu 

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv Mwanza

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa imesema inafanya kazi ya kudhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata Dawa na Vifaa vyenye ubora,Usalama na Ufanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotelembelea Mamlaka hiyo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya  Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Sophia Mziray amesema kuwa, Mamlaka hiyo imekuwa na ufatiliaji dawa katika mnyororo mzima wakati inaingia na wakati usambazaji kutoka chanzo kikuu  kwenda kwa watumiaji.

Hata hivyo amesema wafanyabiashara wafuate taratibu kwani hawawezi kupitisha dawa na ikaendelea kuumiza wananchi na kusema kuwa wamejipanga kila sehemu ya mipaka.

 Mziray amesema kuwa udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba unahitaji ushirikiano na wadau mbalimbali kwani madhara yatokanayo na Dawa  haliwezi kugusa mtu mmoja Bali litagusa watu wote kutokana dawa ilivyosambaa.

Amesema Kanda ya Ziwa ina Mikoa Sita pamoja na mipaka  katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo bila kuwa na utaratibu wa kufatilia uingizaji wa Dawa kunaweza kutoa mwanya kwa wafanyabiashara kuingiza dawa bandia ,au zilizoisha muda na kuleta madhara katika jamii.

Mziray amesema kutokana na Ofisi ya Kanda ya Ziwa kuwa Mwanza wameweza kusogeza huduma Bariadi mkoani Simiyu ambapo watahudumia Mikoa ya  Kanda ya Ziwa Mashariki.

Amesema wamekuwa na ukaguzi aina tofauti ukiwemo ukaguzi elekezi wa majengo mapya ya kutengenezea daw a,Uhifadhi wa dawa, Vifaa Tiba pamoja na vitendanishi kwa kutoa ushauri wa kitaalam kabla kuanza uzalishaji.

Amesema kuna ukaguzi wa kawaida katika kujihakikishia kuwa bidhaa zinaendelea kuzalishwa, kuhifadhia kwa kutoa utaratibu zikiwa na ubora, salama na  zenye ufanisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...