TAMASHA kubwa lililopewa jina la Pamoja ambalo limeandaliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania linatarajia kufanyika Januari 28 mwaka huu katika Viwanja vya Kituo cha Utamaduni cha Alliance de France jijini Dar es Salaam.
Katika tamasha hilo mbali ya kuwepo kwa mdahalo kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kimaendeleo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii na wanamuziki ambao watatumbuiza siku hiyo pamoja na kutoa elimu kwa jamii kupitia tasnia ya sanaa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo, Balozi
wa Ufaransa nchini Tanzania Frederick
Clavier amesema ubalozi huo kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii na wanamuziki
hapa nchini wameandaa tamasha hilo
ambalo kabla ya burudani kutakuwa na mdahalo.
Amefafanua Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kila inapofika Alhamisi ya mwisho wa Januari kupitia Kituo chao cha Utamduni cha Alliance de France pamoja na taasisi zake huandaa tamasha hilo na mwaka huu litafanyika Januari 28.Pia tamasha hilo litahusisha wasanii wa sanaa ya uchoraji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake Msanii kutoka bendi ya Bahati Pili Maguzo, ametumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kufika kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo litatoa burudani na wakati huo huo kujengeana uwezo kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
"Tunaomba wananchi wengi kufika katika tamasha hili ambalo wenzetu wa Ubalozi wa Ufaransa wameaua kuliandaa kwa nia njema ya kuhakikisha kwanza tunaedelea kudumisha tamaduni zetu lakini pia kujengeana uwezo wa masuala mbalimbali kupitia mdahalo ambao utafanyika siku hiyo.
"Tunatarajia kuwa na watu wengi, wanafunzi kutoka Vyuo Vikuu zaidi ya 200 watashiriki, ni tamasha kubwa na la aina yake.Tunaamini katika siku hiyo kutakuwa na mambo mengi ya kujifunza pamoja na kupata burudani kutoka kwa wasanii,"amesema.
Wakati huo huo Mwanamuziki wa kujitegemea Jaffary Bandokine ameeleza
amejiandaa vya kutosha kuelekea katika tamasha hilo na siku hiyo ataimba nyimbo
mchanganyiko zikiwemo za Tanzania na nchi za Magharibi.Imeelezwa katika mdahalo
huo Mjasiriamali na Mfanyabiashara Nancy Sumari ni mmoja ya wageni waalikwa
ambao watatoa mada kwa vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...