Kaimu Mkurugenzi Mkuu toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akiwasilisha mada katika kikao kazi nawataalam wa Kilimo na Ushirika Mkoani Singida
Godwin Mutahangarwa Mwanasheria kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akiwasilisha mada i nayohusu Sheria ya Kilimo cha Umwagiaji ya mwaka 2013 na kanuni zake katika kikao kazi na wataalam wa kilimo Mkoani Singida.
Picha ikionesha Sehemu ya washiriki katika kikao kazi hicho |
Washiriki wakifuatilia kikao kazi kilichohusisha wataalam wa Kilimo na Ushirika Mkoani Singida
Na Mwandishiwetu - Singida
Maafisa
Kilimo Ushirika na Umwagiliaji Mkoani Singida, wametakiwa kuzingatia
nakutumia kikamilifu Sheria ya Taifa ya Umwagiiaji ya mwaka 2013 na
kanuni zake pamoja na Sheria ya usimamizi na uhifadhi wa Mazingira ya
mwaka 2004,ilikuweza kunusuru na kulinda vyanzo vya maji,nakutunza
Miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji.
Hayo yamesemwa leo na
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali,
alipoikuwa akizungumza katika kikao kazi na maafisa kilimo ushirika na
wahadisi wa Umwagilijiaji Mkoani Singida.
Bw. Kaali amewataka
wataalam hao wazielewe sheria hizo na kuhakikisha zinafanyakazi na
kueleweka kwa umma na bila kupepesa macho kuwe na utii washeria bila
shuruti na kuwachulia hatua wale wote wanaofanya uharibifu wa mazingira
kwa kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji,ilikulinda
miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
“Ni lazima kuzingatia
utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo,nauchafuzi wa miundombinu
ya umwagiliaji, mshirikiane na mamlaka husika ili kuweza kunusuru
mazingira na kutunza miundombinu hiyo na mazingira,iko wazi kabisa kuwa,
miundombinu mingi iliyoharibika inaonekana kuwa chanzo kikubwa ni
uharibifu wa mazingira.” Alibainisha.
Akiongelea suala la
Uhabirifu wamazingira litokanalo na mabadiliko ya Tabianchi, Bw. Kaali
amesema ili kuhimili na kukabiliana na changamoto hiyo, wamekuwa
wakihamasiha matumizi sahihi ya teknolojia nyingine sambamba na kupanga
mikakati ya pamoja ya kuelendeleza sekta ya kilimo cha umwagiliaji kwa
kushirikiana na sektabinafsi.
Akiongea katika kikao kazi hicho,
Bw. Suleiman Musunga Afisa Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji toka Wilaya ya
Mkalama ameushukuru Mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika nakuongeza
usalama wa chakula katika maeneo kame nchini, (Reversing land
Degradation trends and increasing food security in degraded ecosystem in
semi-arid areas of Tanzania) Unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira ,Kwa kukamilisha hatua ya awali ya kazi ya upembuzi yakinifu
na nakuelekea kwenye hatua nyingine ya ujenzi wa mabwawa.
Mradi
ambao utawawezesha wakulima katika eneo hilo kuweza kupata maji salama
kwa ajili ya kilimo,na wafugaji kwa ajili ya mifugo na matumizi ya jamii
iinayoishi maeneo kame.
Kikao kazi hicho cha siku tatu,
kilihusisha wataalam wa sekta ya kilimo na umwagiliaji kutoka katika
Manispaa ya Singida na wilayaza Manyoni,Ikungi,Itigi,Iramba na Mkalama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...