WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amemuagiza Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Magembe kuandaa vyeti  kwa ajili ya kuwatambua watumishi watano wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini.

Waziri Dkt. Gwajima amesema atawatambua watumishi hao kwa kusaini vyeti vyao kwa kugusa matarajio yake na kuwatia moyo katika utendaji kazi na kuwa wawazi katika kuleta maendeleo ya hospitali zao hususani kwenye uboreshaji wa utoaji huduma za afya pamoja na usimamizi wa mapato kwenye maeneo yao.

Aliwataja watumishi hao wanatoka hospitali za rufaa za mikoa ni  Bi. Uyanjo Nkumbi-Matroni(Seketoure), Bi. Juhudi Nyambuka-Afisa Afya (Temeke) pamoja na Bi. Adelina Ilongola-Afisa Muuguzi Msaidizi Mwandamizi, Nicolaus Okoth-Afisa Muuguzi Msaidizi na Mohamudu Ramadhani- Mhasibu Msaidizi wote wa Kitete.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...