Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Samson Rweikiza ameshiriki katika Harambee ya Uchangiaji wa Ujenzi wa Kituo Cha Afya Kinachojengwa chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika eneo la Ruhija Kata ya Ibwera Halmashauri ya Wilaya Bukoba Februari 21, 2021.

Harambee hiyo iliyowashiriksha Wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Serikali na Siasa imefanyika ikiwa ni siku ya Tatu ya maombi Maalum Kuombea Taifa kufuatia Hali ya magonjwa yanayoendelea hivi Sasa, ambapo pamoja na Mambo mengine imeombwa Dua Maalum ya kuliombea Taifa kuondokana na Magonjwa hayo.

Katika Risala iliyosomwa mbele ya Mheshimiwa Mbunge Rweikiza, Ujenzi Kituo hicho Afya tayari umekamilika msingi kwa Baadhi ya majengo, na kwamba Ujenzi utaendelea kwa Hatua inayofuata ya kunyanyua Kuta, huku gharama za Ujenzi mzima kukamilika kwa Kituo hicho ikikadiriwa kuwa zaidi ya Shilingi Milioni 140.

 Akijibu Risala hiyo Mhe. Rweikiza amepongeza kwa Hatua Kubwa zilizofanywa na Baraza Hilo la Waislamu kwa wazo lao la kujenga Kituo hicho Afya, ambapo amenukuliwa akisema, "..kujenga Kituo Cha Afya Ni Jambo kubwa lakujivunia na kusifiwa hata Kwa Mungu, nawaombeni mjitolee mjenge Kituo hiki kimalizike.." amesema Dkt. Rweikiza.

Aidha amewaomba na kuwasititiza Waislamu hao kuwa wasiwe na fikra za kushindwa katika Jambo la Hilo la Heri na kwamba ataendelea kuwaunga Mkono na kuwatafuta Wadau wengine wa kuchangia.

Katika Harambee hiyo,   jumla ya Shilingi Milioni Sita zimepatikana ikiwemo ahadi pamoja na pesa Taslimu shilingi Milioni 2.53, katika pesa hiyo Mhe. Mbunge amechangia Shilingi Milioni moja Taslimu na ahadi ya mabati ya kuezekea ya Shilingi laki Tano Licha ya michango mingine iliyokwishatolewa na Mbunge huyo.

Mhe. Rweikiza (Mb) Bukoba Vijijini akiteta Jambo na Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaji Haruna Abdallah Kichwabuta wakati wa Harambee ya Uchangiaji Ujenzi wa Kituo Cha Afya Ruhija Kinachojengwa Kata ya Ibwera
Sheikh wa Wilaya Bukoba Vijijini Sheikh Twahir akiongoza Meza Kuu kutembelea Msingi wa Kituo Cha Afya Ruhija uliokamilika ili kujionea shughuli ilipofikia kwa Sasa

Mgeni Rasmi na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Dk. Jason Samson Rweikiza akiongea wakati wa Harambee ya Uchangiaji wa Ujenzi wa Kituo Cha Afya Ruhija Iliyofanyika Kata ya Ibwera Jimboni humo.
Katibu wa Mbunge na Diwani wa Kata Kaibanja Mhe. Jason Rwankomezi akitoa mchango wake wa kuchangia Ujenzi mbele ya Mgeni Rasmi
Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro akitoa Salaam kwa Niaba ya Serikali

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...