MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wanamshikilia mwanaharakati Joyce Kiria kwa kosa la kuendesha mtandao wa Youtube bila kuwa na leseni.
Hatua hiyo ni muendelezo wa Mamlaka hiyo katika kudhibiti Mawasiliano kwa watu wanaondesha maudhui kwa njia ya Mtandao, pamoja na kutoa elimu kwa watu wanaoendesha maudhui mtandaoni kujisajili katika Mamlaka hiyo.
Mbali na Joyce Kiria TCRA kwa kushirikiana na polisi wamemkamata mtu mmoja kwa kuendesha Chaneli ya Youtube bila usajili.
Joyce Kiria anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi Mabatini Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...