Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -ARUSHA
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta amemshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muunganano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutoa ndege ya serikali kubeba
mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega
kuelekea kwenye maziko jijini mwanza.
Akitoa
ratiba ya kuaaga mwili kwa waandishi wa habari, Kimanta alisema kuwa
Rais Magufuli ameonesha kuthamini utendaji wake wa kazi na ameonesha
heshima kubwa kwa kiongozi mwenzao.
Alisema
ratiba ya kuaga na kuelekea kwenye maziko itaanza kesho Ijumaa
asubuhi ambapo majira ya 7:50 mwili utachukuliwa katika chumba Cha
kuhifadhia maiti na kupelekwa nyumbani kwake na baada hapo wataondoka
nyumbani na kwenda katika kanisa la mtakatifu Theresa kwa ajili ya misa.
Alisema Misa itaanza saa mbili kamili asubuhi hadi saa tatu na baada ya hapo
wataondoka kuelekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya hotuba ya Mkuu wa mkoa na Salamu mbalimbali za rambirambi ambazo zitaambatana na
kuaga mwili wa marehemu na zoezi hilo litaanza saa 9:25 asubuhi hadi
saa 1:30 mchana na baada ya hapo maandalizi ya kwenda uwanja wa ndege wa
Arusha yataanzaa na wanatarajia kuondoka majira ya saa 3: 00 alasiri
kwenda mwanza.
Alifafanua
kuwa baada ya kufika jijini Mwanza mwili utapelekwa nyumbani kwake
Buswalo ambapo utalala hadi asubuhi, ambapo majirani watapata wasaa wa
kuaga na baada ya hapo wataelekea Wilaya ya Sengerema Katika kijiji cha Ngoma
ambapo ndiko alipozaliwa kwa ajili ya ibada na maziko ambayo yatafanyika Alasiri siku ya Jumamosi.Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mhe. Iddi Kimanta
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...