Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -ARUSHA
MBUNGE wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo jana amegawa bima za afya za mfuko wa jamii NHIF 100 kwa watoto wenye ulemavu waliopo Katika jiji la Arusha.
Akiongea wakati wa kukabidhi bima hizo za afya mbunge huyo alisema kuwa nia kutoa bima hizo ni kuweza kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum kupata huduma ya afya uhakika na kirahisi katika Vituo mbalimbali vya afya vilivyopo apa nchini .
Alisema hii ni ahadi moja wapo ambayo ameitekeleza wakati alivyokuwa akifanya kampuni Katika kipindi cha uchaguzi ,huku akifafanua kuwa mbali na kugawa bima hizo za afya pia alishagawa viti vya mwendo (wheelchairs) kwa watoto 100 wenye tatizo ulemavu.
Alibainisha kuwa huo sio mwisho wa kusaidia watoto na kufafanua kuwa bima hizo zitakapoisha atachangia tena kwa mwaka mingine,au wananchi ataendelea kuwasaidia kadri awezavyo kwani waliweza kumuamini na kumtuma akawakilishe bungeni na kuwapelekea kero zao ili ziweze kutatuliwa.
"Pia leo nimesikia mzazi mmoja analalamika kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikiwakataa kuwapokea na kuwandikisha watoto wenye ulemavu,wengine wamekuwa wakiwaambia wazazi wawapeleke watoto kwenye shule zenye utindio wa ubongo hii hali mtoto uyo akiwa anasumbuliwa na tatizo la miguu mimi niseme tu suala hili nilikuwa sijalipata ndio nimelipata .....niwaaidi nitalifanyia kazi,nitalifikisha kwa viongozi wenzangu akiwemo mkurugenzi wa halmashauri , madiwani pamoja na mkuu wa wilaya Ili tuone ni namna gani tunaweza kutatua sala hili kwani ni haki ya kila mtoto kupata elimu."alisema Gambo .
Kwa upande wake mmoja ya mzazi aliepata msaada huu Asha Ally alimshukuru Sana mbunge kwa kuwajali watoto wao na kusema kuwa awali walikuwa wanateseka sana haswa pale mtoto akiumwa na unakuta mzazi ana fedha za kumpeleka mtoto hospital hivyo bima hizo zitawasaidia Sana.
Zainabu aliomba serikali isaidie shule zenye watoto wenye ulemavu kuwajengea mazingira rafiki ya miundombinu Kama vyoo ,madarasa yao ambayo wataweza kunihudumia wenyewe pamoja na njia zao,ambapo pia aliongeza kuwa serikali iwadaidie kuwaelimisha walimu kuwa pokea watoto wenye ulemavu haswa wale wenye ulemavu wa viungo Kama miguu kwani nao wanawajibu wa kujipatia elimu
Naye mganga mkuu wa jiji la Arusha Dr.Kheri Kagya alisema kuwa jiji la Arusha Kuna watu zaidi ya 500 wenye ulemavu wa aina mbalimbali,wao Kama jiji wapo kwenye mkakati wa Kuhakikisha watu hao wanapata huduma staiki ambapo alisema kuwa wanampango wa kuwaita walemavu wote na kuwapa elimu ya Mkopo na ikiwezekana waanze kuwapa mikopo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...