Katika kuelekea sikukuu ya Valentine Day (SikuyaWapendanao) watu mbalimbali wamekuwa na kawaida ya kuitumia siku hii kufurahia na wapendwa wao kwa kuwa nao karibu na kuwapatia zawadi mbalimbali kama sehemu ya kuonesha umuhimu na jinsi wanavyowajali wapendwa wao. Leo tarehe 04/02/2021 katika ukumbi wa Mikutano wa Maendeleo Bank iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Meneja wahuduma kwaWateja wa Maendeleo Bank Sylvia Chaula, amezindua rasmi kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*52#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank.
Sylvia Chaula ameeleza kuwa kilele cha kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO kitakuwa ni siku ya wapendanao (Valentine’s day) yaani tarehe 14/02/2021 ambapo washindi watatu watakaoshinda watapata zawadi mbalimbali kama vile Laptop, Simu Janja, Saa pamoja na kupata chakula cha usiku naMkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr Ibrahim Mwangalaba pamojana jopo la wafanyakazi wa Maendeleo Bank katika Hotel ya Holiday Inn iliyopo Posta. Washindi wote watatu watapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakujana +plus one wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usiku pia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka Maendeleo Bank. Aliongeza Sylvia Chaula. Unajua maneno matupu hayanogeshi shughuli, siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Bank tunapenda kutumia muda wetu kuwaonyesha wateja wetu kuwa tunawapenda, tunawajali na kuwathamii ndio mana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha wateja wetu upendo tulionao kwao kwa vitendo na sio maneno.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...