Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni, Mohamed Bushir akizungumza na wazazi,walezi leo tarehe 4 Februari 2021. katika mkutano wa kujadili masuala mbalimbali kuhusina na maendeleo ya shule, mkutano ulifanyika katika shule ya Sekondari ya Njechele ambapo ameziomba mamlaka za juu kusaidia umaliziaji wa bweni la wanafunzi wa kike ambao wanatoka maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam kuja kusoma katika shule hiyo ambayo imekuwa ya nne kwa wilaya ya Kinondoni kwenye matokeo ya kidato cha nne.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni, Mohamed Bushir akiwa ameambatana na wazazi na walezi baada ya mkutano kumalizika wakikaguwa jengo la bweni ambalo halijakamilika kwa kukosa vitanda uzio na vitu mbalimbali leo tarehe 4 Februari 2021. Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Njechele,Dickson Kajuna akizungumza na Michuzi Tv ambapo amesema shule yake imekuwa ya nne kiwilaya kwenye matokeo ya kidato cha nne na endapo mabweni yakikamilika shule hiyo itakuwa ya kwanza kwakuwa wanafunzi wa kike hawatasafiri umbali mrefu, leo tarehe 4 Februari 2021. Jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Jengo la Mbweni la Shule ya Sekondari Njechele kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wazazi na walezi wakimsiliza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mbopo kata ya Mabwepande wilaya ya Kinondoni,Mohamed Bushir.(Picha na Emmanuel Massaka, Michuzi TV.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...