Na Woinde Shizza ,Michuzi Tv-ARUSHA
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwira amewataka madereva kufuata
sheria ,kanuni za barabarani ,Ili kulinda usalama wao wenyewe , abiria
pamoja na wanaotumia barabara .
Aliyasema
hayo leo Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakati wa
zoezi la kuuaga mwili wa aliyekuwa katibu tawala mkoa wa Arusha Richard
Kwitega aliyefariki dunia February 3 mwaka huu kutokana na ajali ya
gari ulipotokea katika eneo la Mdori lililopo wilaya Babati mkoani
Manyara.
Alisema kuwa
asilimia kubwa ya ajali hii iliyoondoa maisha ya Kwitega imesababishwa
ukiukwaji wa sheria za barabarani za madereva hivyo nivyema madereva
wakajitaidi kuchukuwa taathari na wajitaidi kulinda usalama wao,usalama
wa abiria waliowabeba na hata wale watembea kwa miguu wanaotumia
barabara.
"Nipende
kuwaambia familia muombeni Mungu na naomba tumuombe Mungu amnyanyue mtu
atakae ridhi mikoba yake ,atakayeweza kufuata nyayo zake na atakaye ziba
pengo lake"alisema Mgwira.
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Iddi Kiman'ta alisema kuwa msiba huu ni mkubwa mno
kwa wana Arusha kwani wote wanafahamu ni namna gani mkoa umekuwa
ukifanya vizuri katika sekta mbalimbali ambapo alibainisha chanzo cha
kufanya vyema ni Kwitega ambaye ndio alikuwa Msimamizi mkuu wa utendaji
wa shughuli za serikali.
"Nasema
haya si kumfurahisha mtu bali nasema uhalisia wake alikuwa ni mtu
ambaye ni mtulizaji wa mambo ,hata kuwepo na jambo gumu kiasi gani
kikifika ofisini kwake litapata ufumbuzi ,alikuwa ni mtu mwenye kujenga
hoja,alikuwa na upendo na mwenye kuheshimu mamlaka hivyo nipende
kusisitiza tuache chuki ,tuache fitina na majungu na tupendane , Richard
nenda , Richard nenda ndugu yangu wengine tupo tunakuja tupo nyuma yako
,nenda kakake upande wa kulia wa baba na sisi tunakuja katuandalie
makao twaja"alisema Kiman'ta.
Kwa
upande mkuu wa mkoa wa Morogoro Lootha Sanare alisema kuwa Kwitega
alikuwa ni zaidi ya kiongozi hapa Arusha hasa wakati ambapo siasa
zilikuwa moto haikubali jambo lolote liharibike au lisiwekwe sawa
,alieleza namna ambavyo serikali inatekeleza ilani ya chama cha
mapinduzi ,lakini pia alifanya kazi Arusha huku akitumika Katika mikoa
mingine.
Nae msemaji wa
familia ya Kwitega ,Christooher Nkisi aliushukuru uongozi wa mkoa wa
Arusha pamoja na Manyara na serikali kwa ujumla kwajinsi walivyoweza
kumsitiri na kumuhifadhi ndugu yao tangu pale alipopata ajali.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha
(APC)Claud Gwandu alisema kuwa kwa kutambua mchango mkubwa wa marehemu
katibu tawala ,katika sherehe za kuazimisha siku ya uhuru wa vyombo vya
habari wanaanzisha tuzo za kiongozi bora , hivyo kwa heshima na kutambua
mchango wake tuzo ya mwaka huu watampa yeye ambaye alikuwa ni mwanga
katika utendaji wa viongozi mkoa wa Arusha .
marehemu
Richard Kwitega alozaliwa agast 15 ,1965 Katika Kijiji Cha Ngoma
wilayani Sengerema mkoani Mwanza ameacha mjane na watoto wanne ,wawili
wa kiume na wawili wa kike.
Mkuu wa mkoa wa
Arusha Iddi Kimanta akitoa heshima za mwisho ya kuaga mwili wa
aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha marehemu Richard Kwitega.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...