Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga akizungumza na  baadhi wananchi.
Mbunge Nyamoga akizungumza na madiwani na wanafunzi wa Shule ya msingi mbigili.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga akikagua moja ya
majengo ya shule ya sekondari Mazombe.

Na Denis Mlowe, Iringa

MBUNGE wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Justin Nyamoga amezipongeza
kampuni ya New Forest, shirika lisilo la kiserikali la Lyra In Africa
kwa kufanikisha ujenzi la bweni la shule sekondari Mazombe.

Ujenzi huo umejengwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa
kata ya Lugalo wilaya ya Kilolo kwa ajili ya wasichana wa Shule ya
sekondari Mazombe waliokuwa wakipata changamoto ya baadhi kukosa
makazi na kupanga uraini.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea wananchi na
kuwashukuru kwa kukichagua chama cha Mapinduzi kwa kura nyingi na
kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo Hilo, Nyamoga alisema moja ya ahadi
zake kuhakikisha sekta ya Elimu inakuwa Katika Jimbo la Kilolo.

Alisema kitendo cha kampuni ya Forest na Lyra in Africa ni Cha kuungwa
mkono kwani inaonyesha ni kiasi gani wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Aidha Nyamoga aliwashukuru wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo
na wananchi wa kijiji cha Mazombe kwa ushirikiano wao mzuri wa kujenga
bweni la wasichana katika shule sekondari ya Mazombe kwani itasaidia
kwa kiasi kikubwa utoro na mimba zisizotarajiwa.


Akizungumzia tatizo Ia maji katika Kata hiyo Nyamoga alisema kuwa
litatatuliwa kwasababu serikali inatekeleza mradi mkubwa wa maji
unaogharimu takribahi shilingi Bilioni 10 za Kitanzania kwa ajili ya
kutatua kero hiyo kwa wakazi wa kata ya Lugalo.

Aidha alisema kuwa ataendelea kushirikiana nao ili kukamilisha ujenzi
wa zahanati ya kijiji cha Mbigili na kufanya ukarabati wa shule ya
msingi Mbigili.

Katika Ziara hiyo Nyamoga alitembelea shule ya msingi Mkawaganga shule
ya msingi Mbigili. zahanati ya Mazombe na zahanati ya Mbigili kwa
lengo la kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo kuweza kuzitatua
kwa kushirikiana na wananchi na serikali kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...