Akijibu swali la Mhe. Machano Othman Said Muwakilishi wa Jimbo la Mfenesini aliyetaka kujua kuhusu changamoto ya ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali amesema katika kipindi cha majaribio mfumo huo ulibainika kuwa na dosari ambazo zimeanza kufanyiwa marekebisho.
Amesema kuwa mfumo huo wa majaribio umewashirikisha wafanyabiashara 150 kutoka makundi tofauti ya biashara Unguja na Pemba.
Waziri Jamal amesema mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika mwezi wa Aprili kwa watu wote waliosajiliwa kulipa kodi na kwamba hivi karibuni itazindua rasmi matumizi ya vifaa vya mfumo wa kutolea riisti za kieletroniki.
Aidha Waziri Jamali amewataka wananchi kudai risiti kila wanapolipa fedha kwa unuuzi wa mafuta ili kuimarisha maendeleo ya nchi na kufikia malengo yake.
Vilevile serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Ofisi ya Mufti imekusudia kufanya uhakiki wa misikiti na madrasa zote za Zanzibar ili kuhakikisha misikiti na madrasa inasajiliwa kwa mujibu sheria na taratibu.
Akijibu suala la Mh Salma Mussa Bilali nafasi za wanawake alietaka kujua serikali imejipanga vipi kuhakisha misikiti na madrasa zote Zanzibar zinasajiliwa.
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utwala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema kwa sasa ofisi hiyo imeshaanza kufanya uhakiki wa madrasa za Mkoa wa Mjini Magharibi na Kaskazini Unguja ambapo zoezi hilo litaendelea Mkoa wa Kusini Unguja na Mikoa yote ya Pemba.
Amesema ofisi hiyo imeeandaa utaratibu wa kufanya ukaguzi wa misikiti na madrasa ili kubaini matatizo yanayozikabili na kuyapatia ufumbuzi kwa kushirikiana na wananchi wenyewe.
Akiuliza suali la nyongeza Mhe Panya Abdalla Nafasi za wanawake alilouliza kwanini walimu wa madrasa baadhi yao hawana taaluma ya kutosha na katika kusomesha na kutaka kujua ofisi hiyo imejipanga vipi.
Waziri Haroun amesema Ofisi ya Mufti imejipanga vizuri katika kuwapa elimu ili kupata walimu bora katika ufundishaji.
Akijibu suala la Mhe Abdallah Abas Wadi Jimbo la Nungwi kutokana na changamoto ya kukosekana kwa maji safi katika Kijiji cha Nungwi na Fukuchani Waziri wa Maji nishati Suleiman Masoud Makame amesema ZAWA inaendelea na zoezi hilo kwa kushirikiana na viongozi wa siasa wajimbo la Nungwi na Mkoa na wasamaria wema ili kuharakisha huduma hiyo ipatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...