Na Shukrani Kawogo, Njombe
Wakulima wilayani Ludewa mkoani Njombe pamoja na wachimbaji wadogo wa madini wilayani humo wamempongeza na kufurahishwa na kitendo cha mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kufikisha kilio chao bungeni juu ya upatikanaji wa reseni na maeneo ya machimbo ya madini pamoja na gharama za mbolea.
Pongezi hizo wamezitoa baada ya mbunge huyo kuchangia hoja ya mipango na Maendeleo ya taifa na kuiomba serikali kufuta reseni za wachimbaji ambao hawaendelezi maeneo hayo na kuwapatia wachimbaji wadogo ambao wanaweza kuendesha maeneo hayo na kuweza kuongeza pato la halmashauri hiyo na taifa kwa ujumla.
“Mhe, Naibu Spika tulipokuwa kwenye Mkutano wa RCC Mkoa wa Njombe watu wa Madini waliwasilisha taarifa kwamba Wilaya ya Ludewa ina jumla ya leseni 104 ambazo hazitumiki zimekuwa zikihuishwa tu, waliomba leseni hizo zifutwe na maeneo hayo yagawiwe kwa Wachimbaji wadogo ili Watanzania, Mkoa wa Njombe na nyanda za juu kusini waweze kuongeza vipato vyao na kipato cha Taifa kwa ujumla” Alisema Kamonga.
Aliongeza kuwa kwenye eneo la Makaa ya mawe kuna leseni kubwa mbili ambazo zote zimeshikiliwa na serikali hivyo kutokana na halmashauri ya wilaya hiyo kukusanya mapato hafifu kutokana na kutoendelea kwa miradi mikubwa ambayo ingewawezesha wananchi wake kufanya biashara mbalimbali na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa pia.
"Mapato ya Halmashauri yetu ni milioni 800 na sisi tulitamani Mhe, Waziri wa Madini angetumegea kidogo eneo la uchimbaji ili tuweze kuwekeza kwenye uchimbaji huo kwaajili ya kukuza pato la Halmashauri yetu tuweze kuhudumia Wananchi nao waweze kuwa na kipato kizuri kwani watafanya shughuli za Biashara hivyo Serikali itapata mapato kupitia kodi” Alisema Kamonga.
Aidha katika upande wa kilimo mbunge huyo amesema wakulima wa jimboni kwakwe wamekuwa wakufanya shughuli hiyo ya kilimo kwa gharama kubwa sana huku mavuno yao hayaendani na gharama walizotumia.
Amesema jimboni kwake mfuko mmoja wa mbolea huuzwa kwa wastani wa Sh. 56,000 hadi Sh. 65,000 huku hekari moja ikitumia mifuko isiyopungua minne na mavuono wanayopata kwa hekari hiyo ni maroba yasiyozidi kumi na kila roba anauza kwa Sh. 40, 000 kitu ambacho mkulima huyo anakuwa hanufaiki kabisa kwa shughuli hiyo kwani pesa aliyowekeza ni nyingi zaidi ya hiyo anayopata.
Pia aliiomba serikali kuweka vituo vya utafiti katika mikoa ambayo watu wake wanajishughulisha na kilimo ambavyo vitakuwa vikifanya uchunguzi wa udongo kwakuwa mwananchi anaweza kutumia Mbolea ambayo wakati mwingine haihitajiki kwenye udongo wa eneo husika.
"Endapo vituo hivi vitawekwa vinaweza kuwafanya wakulima kulima kilimo chenye tija kwani vituo hivi bikiwa vyenye uwezo zaidi vinaweza kutoa taarifa nzuri na taarifa hizo zisibaki kwenye makablasha bali washirikishe wataalamu wa Kilimo wa halmashauri zetu ili kusaidia katika kukuza Maendeleo". Alisema Kamonga.
Nao baadhi ya wakulima wa wilaya hiyo wamesema wanaimani kuwabwa na mbunge wangu kuwa atawakomboa kutoka katika kilimo duni wanachokifanya sasa na kuwafikisha katika kilimo chenye manufaa zaidi huku wachimbaji wadogo nao wakimshukuru kwa kurikisha kilio chao cha muda mrefu kwani hawapendezwi kuona reseni zikishikiwa bila kufanyiwa kazi huku wao wakiwa na utayari wa kufanya kazi hizo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akichangia hoja ya maendeleo ya taifa akiwa bungeni.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini wakieleza kwa jinsi gani wanatamani kupatiwa reseni za uchimbaji huo
Baadhi ya mawe yenye madini ndani yake ambayo yanamilikiwa na wachimbaji wadogo
Baadhi ya vibanda ambavyo humilikiwa na wachimbaji wadogo wa madini katika eneo la mkomang'ombe wilayani Ludewa mkoani Njombe
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...