Kaimu
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt.
Julieth Magandi (kushoto) akizungumza wakati wa kupokea msaada wa mashine ya
kufanyia uchunguzi wa macho (Slit Lamp Biomicroscope),
katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho Muhimbili-Mloganzila Catherine akifuatiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Vision Care
Bw. Taegyun Kim
HOSPITALI ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila imepokea msaada wa mashine ya uchunguzi wa macho (Slit
Lamp Biomicroscope) yenye thamani ya takribani TZS. 20Mil ambayo itatumika
kufanya uchunguzi kwa watu wenye matatizo ya macho.
Msaada huu umetolewa na Taasisi
ya Vision Care inayojihusisha mapambano dhidi ya matizo ya upofu duniani.
Akipokea Msaada huo kwa
niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili -Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema mashine hiyo itasaidia
utendaji kazi katika Idara ya Magonjwa ya Macho.
“Msaada
huu umekuja wakati muafaka kwani mashine hii tunaihitaji hivyo uwepo wake utaongeza
tija katika huduma zetu, tunawashukuru sana kwa kuendelea kuboresha sekta ya
afya Mloganzila”amesema Dkt. Magandi.
Kwa upande wake Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Macho Muhimbili-Mloganzila Catherine Makunja amesema mashine
ya Slit Lamp Biomicroscope ni muhimu kwani kila mgonjwa anayefika kupata huduma
katika Kliniki ya Magonjwa ya Macho lazima apimwe kwa kutumia mashine hii.
“Mashine hii inasaidia
kukuza jicho na kumuwezesha daktari kuona kinachoendelea ndani ya jicho kwakuwa
jicho ni kiungo kidogo” amefafanua Dkt. Makunjna.
“Katika Kliniki ya
Magonjwa ya Macho Mloganzila, kwa mwezi tunawaona wagonjwa 290 hadi 380 ambapo kila
mgonjwa lazima apimwe na mashine hii” amesema Dkt. Makunja.
Kwa mujibu wa Dkt.
Makunja tatizo la macho limeongezeka kwa sasa kutokana na madiliko ya mfumo wa
maisha na watu wengi kutokuwa na uelewa mpana juu ya magonjwa hayo, matatizo
makubwa zaidi ni ya miwani ikifuatiwa na mtoto wa jicho ambayo husababisha
upofu.
Naye Mkurugenzi wa
Taasisi ya Vision Care Bw. Taegyun Kim amesema wataendelea kushirikiana na
Muhimbili katika kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...