*Yafungua milango kwa watanzania kufuga kibiashara na kisasa

Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv 

Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited (NARCO) imesema kuwa kuanzia sasa limeweka tozo moja ya sh.3500 kwa ekari  ndani ya mwaka kwa mikataba mipya ya  upangishaji wa vitalu kwa ajili ya kufanya ufugaji wa kibiaashara na Kisasa.

Tozo hizo hazitahusu wale wenye mikataba ya zamani ni mpaka pale wataporekebisha mikataba yao na kuanza kulipa tozo hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi wa Kampuni Paul Kimiti amesema kuwa kuweka Tozo moja ni agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa mkoani Kagera alipotembelea Mmoja ya mwekezaji moja ya Ranchi mkoani humo.

Amesema licha ya kuweka Tozo amewataka wananchi wawekeze katika ufugaji wa Ranchi kwani maeneo mengi na hayana kugombania malisho kutokana utaratibu ulivyowekwa wa kuwa na malisho ya Kisasa.

Amesema wawekezaji waliopo ni zaidi ya 200 ambao hata robo ya ardhi ya ranchi haijafikia  katika eneo hilo. 

Amesema tozo hizo ya mikataba mipya ya uwekezaji itahusisha Ranchi 14 zilizopo katika Mikoa Tisa ya Tanzania Bara ambazo ni Kongwa iliyopo Dodoma,Ruvu mkoani Pwani, Mkata ,,Dakawa Morogoro,Kalambo Rukwa,West Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro, Mzeri Hill Tanga,Missenyi,Kitengule mkoani Kigoma,Mabale na Kikulula  mkoani Kagera,Uvinza Kigoma, Usangu Mbeya zote zikiwa na jumla ya hekta 627,164.

Nae Meneja wa Masoko wa NARCO Emmanuel Mnzava amesema kuwa uwekezaji huo watu wenye Ng'ombe wawili wanaweza kuunda kikundi na kupata Ranchi kwa ajili ya kufanya ufugaji wa kibiaashara na kisasa.

Amesema milango ipo wazi kwa watanzania kuwekeza katika ufugaji kwani ardhi ni kubwa.
Amesema ufugaji wa kisasa ni ule Ng'ombe akiwa na umri mdogo kuwa na kilo nyingi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited (NARCO) Paul Kimiti  akizungumza akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na mikakati mbalimbali za Ranchi nchini ,jijini Dar es Salaam.


Meneja Masoko wa NARCO Emmanuel Mnzava akizungumza kuhusiana taratibu za mtu kufanya uwekezaji wa ufugaji katika Ranchi zilizopo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...