Na Mwandishi wetu, Simanjiro
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imefanikiwa kupata sh270 milioni
baada ya kufanikisha ukamilishaji wa miradi sita ya maji na usafi wa
mazingira mashuleni.(Swash).
Halmashauri
hiyo imefanikiwa kuwa ya kwanza mkoani Manyara, kati ya halmashauri
saba kwani imeongoza kwenye miradi sita miongoni mwa miradi saba
iliyotolewa kwa kila halmashauri hizo.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi
akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, amewapongeza wataalamu,
madiwani na kamati zilizosimamia miradi hiyo.
Myenzi
amesema baada ya halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kuongoza kwenye
mkoa wa Manyara, itapatiwa fedha hizo sh270 milioni ili kufanikisha
miradi mingine.
Amesema
hiyo ni hatua kubwa kwani halmashauri nyingine hazikukamikisha miradi
hiyo kwa wakati ndiyo sababu wao wakaongoza kwa kukamilisha miradi sita
kati ya saba.
"Mkuu wa
mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti alitembelea moja kati ya miradi hiyo
hapa Simanjiro kwenye eneo la Ngage na kuagiza wenzetu wengine waje
waige mfano hapa kwetu ubora wa miradi," amesema Myenzi.
Amesema
fedha hizo kutoka kwa wafadhili zitachangia kufanikisha miradi mingine
ili kuhakikisha wanaondokana na magonjwa ya milipuko kutokana na hali ya
usafi uliopo.
"Hivi sasa
tunataka magonjwa yote ya milipuko ikiwemo kipindupindu inakuwa
historia kutokana na hali ya usafi wa mazingira na kuwepo kwa vyoo,"
amesema Myenzi.
Amesema
fedha zilizotengwa kwenye miradi hiyo zilitumika ipasavyo katika usafi
wa mazingira, uboreshaji wa maji na ujenzi wa vyoo ili kuondokana na
maradhi.
Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Baraka Kanunga amempongeza Myenzi
kwa namna anavyosimamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Mkurugenzi
wetu Myenzi tunapaswa kumpongeza kwani amekuwa kiranja wa kusimamia
miradi ya maendeleo ipasavyo hivyo tumuunge mkono kwa maslahi mapana ya
wana Simanjiro," amesema Kanunga.
Hata
hivyo, amesema anashukuru ushirikiano anaoupata kupitia mkuu wa wilaya
hiyo, mhandisi Zephania Chaula, Katibu Tawala, Zuwena Omary, mbunge wa
Jimbo Christopher Ole Sendeka na Mkurugenzi Myenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akizungumza kwenye kikao cha
Baraza la Madiwani, kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Baraka
Kanunga Laizer na Katibu Tawala Zuwena Omary Jiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...