Katika kipindi cha muhula wa pili wa miaka mitano ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Tanzania itajikita zaidi katika diplomasia ya uchumi,kuimarisha sekta binafsi,kukuza biashara pamoja na mahusiano na Mataifa mengine duniani.
Msimamo huo wa Tanzania umetolewa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Tanzania na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa na kuongeza kuwa ni dhamira ya Tanzania kuhakikisha kuwa ina uwezo wa kukuza biashara na kuuza bidhaa katika nchi mbalimbali duniani……Prof. Palamagamba John Kabudi
Prof. Kabudi amewaambia Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa Nchini kuwa hali ya kisiasa na amani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla imeimarika kuliko wakati wowote hususani mara baada ya uchaguzi mkuu uliomalizika Octoba,2020 na kwamba uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inachochea kuongezeka kwa uwekezaji na ufanyaji wa biashara kwa lengo la kukuza uchumi.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi Dkt. Ahmada El Badasui `fakih ambaye pia ni Balozi wa Comoro hapa nchini ameshukuru kwa uwepo wa mkutano huo ambao unaowapa fursa mabalozi kufahamu masuala mbalimbali yanavyoendelea hapa Nchini huku Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe Manfredo Fanti akiipongeza Tanzania kwa kuingia uchumi wa kati na kwamba Umoja wa Ulaya uko tayari kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha Uchumi wa Tanzania unaendelea kukua………Mhe. Manfredo Fanti,Balozi wa EU
Mkutano
huo wa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa umehudhuriwa pia na
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe
William Tate Ole Nasha,Katibu Mkuu Balozi,Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge na Wakurugenzi na Wakuu wa Idara na vitengo vya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...