Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

BAADA ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuagiza kuwaondolea vikwazo Wawekezaji kutoka nje ya nchi, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kuwarejesha nchini Wawekezaji wa Kampuni ya ElSewedy ya nchini Misri inayojenga Kiwanda cha Vifaa mbalimbali vya Umeme katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ziara katika eneo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Dkt. Maduhu Kazi amesema Kituo hicho kiliongeza jitihada kuhakikisha Mwekezaji huyo anapatiwa Ardhi hiyo ili kufanikisha uwekezaji huo na mahitaji mengine.

“Hapa katika eneo hili watazalisha Vifaa vya Umeme na Taifa letu litafaidika na uwepo wa Kiwanda hiki kitakachozalisha Vifaa hivyo, pia tutapata Pato la Taifa kupitia uwepo wake na ziada ya kuuza Vifaa hivyo nje ya nchi na kupata fedha za kigeni”, amesema Dkt. Maduhu 

Dkt. Maduhu amesema Kiwanda hicho kitaleta maenedeleo makubwa kwa kuweka Makao Makuu ya Uzalishaji wa Vifaa hivyo kwa eneo la Afrika Mashariki na Kati. “Wataleta Teknolojia mpya ya kutumia Roboti ambayo itahusisha utengenezaji wa Matenki ya Transfoma ambayo itahitaji umakini wa hali ya juu”, ameeleza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya ElSewedy Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Ibrahim Qamar amesema wamekuja kwa Uwekezaji nchini Tanzania kutokana na ushirikiano mzuri waliopewa na Kituo cha Uwekezaji (TIC).

“Bodi ya Kampuni yetu ya ElSewedy imeamini nchi ya Tanzania kuwa na Soko kubwa sambamba na ushirikiano wa Serikali yake katika suala la Uwekezaji.

“Tulienda Kenya, Rwanda na nchi nyingi lakini tuliona Tanzania inatufaa zaidi katika Uwekezaji huu, kwa kweli Mkurugenzi wa TIC ametusaidia sana kuhakikisha tunapata nafasi ya Uwekezaji hapa”, ameeleza Qamar.

Naye Mkurugenzi Mendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka amesema uwepo wa Kiwanda hicho utanufaisha Shikrika hilo kutokana na kuhitaji zaidi Vifaa hivyo vya Umeme. Amesema Shirika litaendelea kutumia Vifaa vinavyopatikana hapa nchini kwa ajili ya Miradi ya usambazaji umeme.

“Tunawaambia ElSewedy kuwa Soko la Vifaa vyao lipo hapa kwetu TANESCO, sisi tutanunua sana Vifaa na miradi mingi zaidi ya Umeme inakuja hapa nchini ili kutanua Mtandao wetu kwa kila mwaka, kuunga Wateja na kuwafikia kwa urahisi”, amesema Dkt. Tito.

Uwekezaji wa Kiwanda hicho umetajwa kuwa wa zaidi ya kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 50 kwa kuanzia na Ujenzi wake kuanza rasmi mwezi June, 2021.

Mkurugenzi wa Kampuni ya ElSewedy Kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Ibrahim Qamar akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na baadhi ya Watendaji wa TIC na TANESCO wakati walipotembelea eneo la Kigamboni kinapojengwa Kiwanda cha Vifaa vya Umeme.
Eneo ambalo kitajengwa Kiwanda cha Vifaa vya Umeme, Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya ElSawedy, Abdel Fattah Ellatar akitoa maelekezo ya ujenzi wa Kiwanda hicho kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Dkt. Maduhu Kazi na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...