NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma bwana Aggrey Mwansasu alitumia siku ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa chama cha mapinduzi na kuwasisitizia viongozi wa vijiji kufuata utaratibu wa uingizaji wafugaji na mifugo yao katika maeneo ya vijiji.
Mwansasu alidai vitendo vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vijiji kuwaingiza wafugaji kinyemera bila kuwashirikisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara kitasababisha migogoro kati ya wakulima na wafugaji siku za usoni .
Mwenyekiti wa chama huyo alitaja kifo cha kijana Mohamedi Athumani Kinunga kijiji cha Matepwende aliyekutwa amekufa porini ni dalili zinazoanza kujionyesha za kuwapokea na kuweka urafiki na watu wasiowajua na waliopokelewa kinyemera bila kufuata taratibu zilizowekwa na serikali alisema mwenyekiti huyo.
Bwana Mwansasu pia aliwataka viongozi waliochaguliwa kuacha kutumia nafasi walizopata kwa kupoteza muda mwingi kupanga safu zao kwa kuwatengenezea mazingira viongozi waliopo katika madaraka waondolewe waweke viongozi wengine wanaowataka kwa kutumia muda mwingi kufanya shughuli hiyo badala ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye Mbunge wa jimbo la Namtumbo mheshimiwa Vitta Rashid Kawawa alianza kwa kuwashukuru wananchi kwa kukipatia ushindi wa kishindo chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana oktoba 2020.
Hata hivyo Kawawa aliwaomba wananchi ushirikianao katika utekelezaji wa miradi, huku akisisitiza kumalizia miradi yote viporo iliyoanzishwa na wananchi kwa kipindi kilichopita na kuanzisha miradi mingine mipya .
Mohamedi Mavallah katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo pamoja na mambo mengine aliwasisitizia waheshimiwa madiwani katika kata zao kupanga ratiba za kusikiliza kero za wananchi katika kata zao na kuzitatua .
Abdulahamani Milanzi (Jangala) mkazi wa kijiji cha Ulamboni kata ya Lisimonji katika shairi lake kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo aliomba ujenzi wa daraja la mto Lukimwa litakalounganisha kata hiyo na kata ya Lusewa, kutengenezewa barabara zakuunganisha vijiji kata hiyo ziweze kupitika muda wote ,
Maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa chama cha mapinduzi miaka 44 iliyopita yalifanyika kiwilaya kijiji cha Matepwende tarehe 3mwezi huu katika kiwanja kilichojengwa mnara wa kumbukumbu ya asili ya Hayati Rashid Mfaume Kawawa aliyekuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...