TOSCI YAWATAKA WAKULIMA KUDAI RISITI NA KUHIFADHI VIFUNGASHIO WANUNUAPO MBEGU.
………………….
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
Kutokana na baadhi ya wakulima kupata hasara inayosababishwa na kununua mbegu za kilimo zisizo na ubora wameshauriwa kununua Mbegu kwenye Maduka yaliyosajiliwa hatua itakayosaidia kupunguza malalamiko ya mbegu zisizo na ubora kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao ya Chakula na Biashara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa mbegu kutoka taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu nchini (TOSCI) Emmanuel Mwakatobe ofisini kwake wakati akiongea na Michuzi Blog iliyofika katika ofisi hizo ili kujua hali ya upatikanaji na ubora wa mbegu katika msimu wa kilimo kwa mwaka 2020- 2021.
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa Mbegu Mkurugenzi mkuu wa mbegu (TOSCI) Emmanuel Mwakatobe ameseme TOSCI imejipanga katika upatikanaji wa mbegu kwa mwaka 2021 na kuwataka wakulima kuacha kununua mbegu katika magulio na sehemu nyingine zisizo rasmi kwa uuzwaji wa mbegu.
Pia amewataka wakulima kudai risiti na kutunza vifungashio vya mbegu husika wanaponunua mbegu, ili watakapouziwa mbegu ambazo hazina ubora waweze kupata msaada kutoka kwa mamlaka ya udhibiti wa mbegu TOSCI na kupata haki zao.

Aidha amewataka wakulima kutoa taarifa za mbegu zisizo na ubora kwa mamlaka ya udhibiti ubora wa mbegu TOSCI ili mamlaka hiyo iweze kuchukua hatua kwa makampuni ambayo hayakidhi vigezo vya uzalishaji na usambazaji wa mbegu kwa wakulima.

Hata hivyo, amewahimiza wakulima juu ya matumizi ya mbegu bora ili kupata mazao yenye tija kwani mbegu bora lazima ifanyiwe utafiti na wataalamu na kuhidhinishwa kwa ajili ya matumizi kwa wakulima.

Kwa upande wao baadhi ya wakulima waliongea na Michuzi Blog wameiomba serikali kupitia taasisi ya kudhibiti ubora wa mbegu nchini (TOSCI) kufanya ukaguzi katika maduka ya kuuza mbegu ili kubaini mbegu zisizo na ubora zinazouzwa kwa wananchi hususani katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo.

Pia wameeleza kuwa wakulima wengi hususani wa vijijini hawajui kusoma jambo linalosababisha kuuziwa mbegu zisizo na ubora, hivyo mamlaka hiyo ikiwa inafanya ukaguzi katika maduka ya kuuzia mbegu mara kwa mara itawasaidia wakulima ambao hawajui kusoma kupata mbegu zenye ubora.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...