Benki ya Exim (Group) imetangaza kupata faida ya jumla ya TZS 25.3 Bilioni (kabla ya kodi) kwa mwaka 2020 ikilinganishwa na hasara ya kiasi cha TZS 8.4 Bilioni iliyopata kwa mwaka uliopita, hatua inayoakisi ukuaji wa asilimia 402%  wa Mwaka hadi Mwaka (YoY).

Mafanikio hayo  yanayotajwa kuwa yametokana na ufanisi wa kiutendaji licha ya changamoto za kiuchumi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ulioathiri ukuaji wa uchumi katika baadhi ya sekta muhimu nchini mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo imebainisha kuwa benki hiyo imetekeleza kwa ufanisi mkubwa mkakati wa kushirikiana na sekta zinazofanya vizuri sambamba na kuongeza umakini zaidi katika matumizi yake ili kuongeza tija zaidi katika utendaji.

“Katika kipindi hicho benki ilikuwa bega kwa bega na sekta zilizoathiriwa wakati wa janga hilo na kwa kweli tulishirikiana kikamilifu na wateja wetu kuhakikisha kwamba si tu tunawapatia fedha bali pia tunawajengea uwezo wa kuweza kufanya shughuli zao katika kipindi hicho kigumu.’’ Alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa wa benki hiyo Bw. Jaffari Matundu.

Kwa mujibu wa Bw Matundu, hadi kufikia tarehe 31 Desemba 2020, benki hiyo ilikuwa imetoa msamaha wa zaidi ya TZS bilioni 290  kwa njia ya likizo ya malipo na upanuzi wa vipindi vya ulipaji wa mikopo ili kusaidia wateja wa benki hiyo ambao biashara zao ziliathirika zaidi na athari za kiuchumi za Covid-19.

"Tunayo furaha kuripoti matokeo mazuri kwa mwaka wa fedha 2020. Tumefanikiwa kurejesha asilimia 9.0 ya faida kwenye mfuko wa wanahisa ikilinganishwa na marejesho hasi ya asilimia 9.2 mnamo 2019" alisema Bwana Matundu katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Nchini Tanzania, benki hiyo ilirekodi mafanikio makubwa kwa kupata faida (kabla ya kodi) ya Shilingi Bilioni 18.8 kutoka kwenye hasara ya TZS Bilioni 14.5 (kabla ya kodi) ya mwaka uliopita.

"Mafanikio hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa  mali kufuatia usafishaji uliofanywa katika kipindi hicho cha mwaka uliopita hatua Iliyosababisha kupungua kwa mikopo chechefu kutoka asilimia 22.3 ya mwaka 2019  hadi kufikia asilimia 7.4 kwaka 2020.''

 "Matawi yetu ya nchini Djibouti na Comoro pia yalirekodi faida ya TZS Bilioni 4.9 na Bilioni 5.7 (kabla ya kodi)  licha ya athari ya COVID-19.

“Jumla ya Mali zetu imebaki kuwa  TZS 1.9 Trilioni. Amana za wateja zimeongezeka kwa 4.4% wakati wa robo ya mwaka na kufikia Shilingi Trilioni 1.38. Shughuli zetu nchini Tanzania, Comoro na Uganda zote zimerekodi ukuaji wa ajabu katika amana za wateja wakati wa robo ya mwisho wa mwaka”aliongeza

Alisema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na kauli mbiu ya benki hiyo "Exim Kazini Leo kwa ajili ya Kesho' ambayo imekuwa ikiisukuma benki hiyo kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja wake.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Bwana Jaffari Matundu (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizungumza kuhusu kuhusu utendaji wa benki hiyo katika kipindi cha mwaka 2020. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Mikopo wa benki hiyo Bi Zainab Nungu, ,  (Kushoto) na Afisa Mkuu Idara ya Fedha Bwana Shani Kinswaga,



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...