KATIKA kuendelea kukuza uchumi wa taifa wanahabari wametakiwa kuendelea kuhabarisha umma kuhusu mchango wa sekta ya viwanda na biashara ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia pato la taifa, na kwa kupitia mradi wa KAIZEN wameshauriwa kutangaza shughuli na fursa zinazopatikana kupitia na mradi huo katika kuelekea siku ya kilele cha KAIZEN nchini itakayofanyika Februari 5 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika semina fupi iliyowakutanisha na wizara ya Viwanda na Biashara, Mratibu wa Mradi wa KAIZEN nchini Jane Lyatuu amesema lengo la mafunzo hayo ni pamoja na kuwaelimisha waandishi kuhusiana na mradi huo pia kutangaza shughuli na fursa zinazopatikana kutokana na mradi huu kuelekea siku ya kilele cha KAIZEN nchini itakayofanyika tarehe 5 Februari, 2021 katika ukumbi wa LAPF Kijitonyama jijini Dar es saalam.
Amesema sekta ya viwanda na biashara imekua ikiendeleza juhudi katika kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora na kwa gharama nafuu na kwa kupitia mradi wa KAIZEN mikoa mingi imekuwa wanufaika kwa viwanda vipatavyo 132 na kuiomba serikali itoe kipaumbele kwa mradi huo ili kuinua zaidi uchumi zaidi.
Siku ya KAIZEN itatanguliwa na Mashindano ya KAIZEN ambayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Tarehe 4 Februari, 2021 na Viwanda vya Tanzania vilivyotekeleza KAIZEN kwa ubora na mafanikio katika nyanja mbalimbali na washindi watapewa zawadi na Waziri wa Viwanda na Biashara siku ya maadhimisho ya KAIZEN tarehe 5 Februari, 2.
KAIZEN ni mradi wa kuimarisha kampuni za uzalishaji na kuboresha ubora na tija, likiwa na asili ya kijapani kwa sasa linatumika duniani kote na katika Wizara ya Viwanda na Biashara KAIZEN inalenga katika kutatua changamoto na kuleta mabadiliko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...