Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival linalolenga watalii kujua vivutio vilivyopo kwenye hifadhi ya msitu wa mazingira asilia wa Kazimzumbwi, tamaduni za Wazaramo na pia kutangaza hifadhi mpya ya Taifa ya Mwl. Nyerere ambapo Kisarawe itakuwa ushoroba kwa watalii kuelekea huko kuona vivutio. Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo (wapili kushoto) na Mhifadhi Mwandamizi Idara ya Utalii wa hifadhi ya Taifa ya Mwl . Nyerere, Seth Mihayo.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Mhe.Jokate Mwegelo akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival litakalofanyika wilayani humo kuanzia tarehe 19 mwezi huu, Tamasha hilo litahusisha matukio mbalimbali ikiwemo tamaduni za Wazaramo, kutembelea msitu wa mazingira asilia wa Kazimzumbwi, Marathon na kutembelea hifadhi mpya ya Taifa ya Mwl. Nyerere.
Mhifadhi Mwandamizi Idara ya Utalii wa hifadhi ya Taifa ya Mwl . Nyerere, Seth Mihayo akizungumza na waandishi wa habari
Mhifadhi Mazingira kutoka WWF, Dkt. SeverIn Kalonga akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...