Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Godwin Gondwe amewataka wamiliki wa Bar na kumbi za starehe kufanya biashara kulingana na vibali wanavyopewa na Manispaa.
Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya Kijamii ndani ya Wilaya ya Temeke.
Akizungumza
na wananchi wa Mtaa wa Moringe Kata ya Mbagala, Gondwe amesema
wamiliki wote wanatakiwa wafuate vibali vyao kama walivyoelekezwa na
Manispaa ili kuondoa kero kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu.
Gondwe
amesema, kila kumbi ya starehe ina kibali chake kuna waliopewa vya
kukesha hadi asubuhi, kuna wengine wamepewa mwisho muda fulani ila wapo
wanaokikuka na ni kosa kisheria.
Amesema,
" Kuna kumbi zinapiga muziki hadi asubuh wakiwa hawana vibali hivyo na
wanatoa kero kwa wananchi kuna wengine ni wagonjwa, wanataka kupumzika
na hili suala nataka watendaji wa mtaa mlifanyie kazi sitaki kusikia
lawama tena za wananchi,"
Gondwe
amesema, kama mmiliki amepewa kibali cha kupiga muziki hadi asubuh
lakini amekuwa anashindwa kufuata masharti yanayotakiwa na kama Manispaa
tukiona mtu anafanya hivyo tutamnyang'anya kibali hicho.
Mbali
na hilo, Gondwe amewataka maafisa Mazingira wa Kata kusimamia mazingira
ipasavyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria wamiliki wa Viwanda
vinavyotiririsha maji machafu kwenye makazi ya wananchi.
Hilo,
ni kutokana na wananchi wa Kata ya Mbagala kulalamika utiririshwaji wa
maji machafu kutoka katika viwanda vilivyopo karibu na maeneo ya
wananchi kikiwemo Kiwanda cha Sabuni.
Aidha, ametoa maagizo hayo kwa viwanda hivyo kuacha haraka tabia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza na
wananchi wa kata ya Mbagala baada ya kupokea malalamiko ya kumbi za
starehe kupiga muziki mkubwa na kuwa kero kwa wananchi sambamba na
uharibifu wa mazingira kutoka kwenye Viwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...