
Picha na Maktaba.
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
WATOTO wanaoishi na kufanya kazi mtaani ni watoto kama watoto wengine na wanahitaji kupendwa, kulindwa na kuwezeshwa kutimiza ndiyo zao.
Hayo yamesemwa na Afisa Mawasiliano wa Shirika la Railway Children Africa (RCA), Henry Mazunda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
"Kama jamii itaendelea kuwabagua, tutatengeneza kizazi cha watu wasio na mchango chanya katika maendeleo ya sasa na badaye." Amesema Mazunda.
Hata hivyo Mazunda ametoa baadhi ya sababu zinazopelekea watoto wengi kutoroka nyumbani kwao kuwa ni pamoja na unyanyasaji na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinatoka katika ngazi ya familia na jamii.
Amesema kuwa katika nyakati ngumu za milipuko ya magonjwa kwa mfano COVID-19, watoto wanaofanya kazi mtaani ni waadhirika namba moja na wanahitaji msaada wetu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
"Kwahiyo ni wajibu wetu sote kama jamii kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapatiwa huduma kama chakula, matibabu na elimu ya kujikinga na magonjwa, pamoja na mahitaji mengine."
Pia serikali ina wajibu kuhakishwa kunakuwepo na sheria na sera Mahususi zinazowalinda watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani." Amesema Mazunda.
Kwa pamoja tunaweza kumaliza au kupunguza kwa kasi kikibwa tatizo hili la watoto wanaoishi na wanaofanya kazi mtaani.
Katika mradi wa USAID- Kizazi Kipya unaotekelezwa na Railway Children Africa kwa kushirikiana na taasisi ya Babawatoto wameweza kutoa msaada wa kisheria, bima za Afya, Chakula huduma ya maji safi, sabuni na elimu ya kujikinga na maradhi, kusoma na kuandika.
Pamoja na hayo Mradi wa USAID- Kizazi Kipya umewasaidia kuwakusanya pamoja katika makundi tofauti ili waweze kupewa mafunzo mbalimbali kwaajili ya kutimiza ndoto zao.
Mratibu wa miradi wa Babawatoto, Johnson Mtango amesema kuwa watoto wanatakiwa kulelewa na baba na mama hivyo jamii ielewe hivyo ili kila mtoto aweze kufaidi haki zake pamoja na kufurahia utoto wake.
Hata hivyo ameiomba serikali itilie maanani hili kundi la watoto na vijana wanaoishi na kufanya kazi mtaani.
Kwa upande wake mmoja wa watoto hao, Emmanuel (Sio) jina lake amewashukuru Taasisi ya Babab watoto kwani wasingekuwa wao angekuwa wameshafariki dunia.
"Unavyoniona hivi Mwandishi (hali yake ya ngozi imejaa mabaka mabaka ya vipele na vidonda) mbona nimepona hawa jamaa wamenisaidia nilikuwa naumwa nusu ya kufa, nililazwa Mwananyamala hospitali pale Babawatoto ndio walinilipia hela ya matibabu mpaka sasa naonekana hivi." Alisema Emmanuel
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Stendi ya Mabasi ya Ubungo, Grace Kasusa amesema kuwa wao kama serikali wanashirikiana na taasisi ya Babawatoto ili kuhakikisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani wanapata haki zao.
Mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, Arusha Iringa na Dodoma inaongoza kwa watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani.
Amesema kuwa taasisi ya Babawatoto inasaidia sana katika kuwashauri watoto wanaofanya kazi mtaani ili waweze kurudi kwao lakini changamo ni pale mtoto ambapo amshazoea mazingira hayo hakubari kurudi nyumbani.
"Sisi tukiwapata watoto tunawaunganisha moja kwa moja na taasisi ya Babawatoto ili wapewe ushauri kwa haraka kwani wakiwa bado wageni ni rahisi kurudi kwao kuliko wale waliozoea katika mazingira ya mtaani." Amesema Grace
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...