Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza jambo wakati wa kikao cha
kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na
sekondari,Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akikazia jambo wakati wa kikao cha
kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za msingi na sekondari,
Kikao hicho kimekutanisha Wizara za Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na Wizara ya TAMISEMI.
Waziri wa Habari.Utamaduni,Sanaa
na Michezo Innocent Bashungwa akieleza mipango mbalimbali ya kuendeleza
michezo wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika
shule za msingi na sekondari, Kikao hicho kimekutanisha Wizara za
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
na Wizara ya TAMISEMI.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Innocent Bashungwa akiteta jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako na Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas mara baada ya
kumaliza kikao cha kujadili namna ya kuboresha michezo katika shule za
msingi na Sekondari, Kikao hicho kimekutanisha Wizara za
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
na Wizara ya TAMISEMI.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Yusuph Singo(kushoto mwenye miwani)
akiwasilisha hoja za wizara yake katika kuboresha michezo katika shule
za msingi na Sekondari Kikao hicho kimekutanisha Wizara za
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia
na Wizara ya TAMISEMI.
Picha na MAELEZO
………………………………………………………………………………………..
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo ametoa agizo kwa Halmashauri zote nchini
kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za michezo, huku akiagiza
Wakurugenzi katika halmashauri hizo kusimamia vyema miundombinu ya
michezo na kuhakikisha maeneo ya michezo hayavamiwi.
Mhe. Jafo ameyasema hayo leo
Februari 08, 2021 jijini Dodoma katika kikao kati ya Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wizara ya
Elimu Sayansi na Teknolojia kilichoandaliwa na Wizara ya Habari ambacho
kilijadili namna ya kuboresha Michezo katika shule za msingi na
Sekondari.
“Nawaagiza walimu wakuu wa shule
zote nchini, kusimamia vyema vipindi vya michezo kwa kuhakikisha
vinafundishwa katika muda sahihi na wanafunzi wanashiriki vyema vipindi
hivyo. Na sisi upande wa Serikali tutasimamia vyema ajenda hiyo na
tutahakikisha maafisa elimu Mkoa na Wilaya wanafuatilia michezo katika
maeneo yao kwakua tunataka Tanzania iwe na wanamichezo wazuri wa
kuisaidia nchi yetu” alisema Mhe. Jafo
Kwa upande wake Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Wizara
yake itahakikisha inaandaaa na kuhuisha Mitaala iliyopo kuhusu somo la
michezo ili somo hilo lilete tija kwa Taifa kwa kuzalisha wataalamu
wengi wa fani hiyo.
“Kwakua tunafahamu Michezo ni
ajira na inajenga afya, ni jukumu letu kuhakikisha tunaisimamia vyema
na tayari katika shule za msingi kuna somo linaitwa Haiba na Michezo na
katika shule za sekondari kuna somo linaitwa Elimu kwa njia ya Michezo
(Physical Education), masomo hayo yanatengeneza wataalamu katika sekta
hiyo” alisema Mhe. Joyce.
Naye Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa mbali na kuzishukuru
Wizara hizo kushiriki na kutoa mawazo chanya yanayolenga kuboresha
maendeleo ya michezo nchini, amesema dhamira ya Serikali ni kuleta uhai
katika timu za Taifa na uhai huo unatokana na kuwepo kwa vipaji
vinavyozalishwa kuanzia shule za msingi na sekondari.
“Sera ya Michezo ya mwaka 1995
ilikua imekosa Mpango Mkakati wa kuitekeleza vyema, na tayari rasimu ya
mpango huo ipo, lengo la kikao hiki ni muendelezo wa utekelezaji wa
vikao mbalimbali vya kuboresha sekta hii kwa kushirikiana na wizara
hizi tatu” alisema Mhe. Bashungwa.
Naye Naibu Waziri wa Wizara ya
Habari Mhe. Abdallah Ulega ametoa wito kwa vyuo na shule zinazofundisha
michezo kusimamia vyema ufundishaji wa masomo hayo kwakua ndio
yanayosaidia kuzalisha wataalam wa kuendeleza michezo nchini.
Kikao hicho kimeazimia mambo mengi ikiwemo kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya shughuli za michezo ya UMISETA na UMITASHUM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...