Msikiti wa Al-Noor Uliojengwa na AL-FIRDAUS Sahare Tanga



Waislam wakiwa ndani wa Msikiti wa Noor Tanga


Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow akizungumza katika Uzinduzi wa Msikiti huo.

JUMUIYA ya Alfirdaus ya Jijini Dar es salaam imeendelea kutekeleza harakati zake za kusaidia jamii ikiwemo uchimbaji wa visima virefu vya maji katika maeneo mbalilmbali hapa Nchini

 

Akizungumza katika ufunguzi wa msikiti Alnoor Uliopo Msakangoto Sahare Jijini Tanga Afisa Mipango wa taasisi hiyo Zack Naseer  Ruqeish amesema kuwa hivi sasa wamefanikiwa kuchimba visima zaidi ya elf saba katika maeneo mbalimbali hapa nchini

 

Zack Amesema kuwa lengo la jumuiya hiyo ni kuisaidia jamii ya kitanzania katika Nyanja mbalimbali za huduma ya Kijamii ambapo kwa hivi sasa wanaendelea na Ujenzi wa jengo  la Waqfu la Ghorofa saba Jijini Dar es salaam ambalo litakuwa ni kitega uchumi cha kuisaidia jamii.

 

Kwa upande wake katibu Mkuu wa Taasisi ya Alfirdaus Saleh Alhinai amesema kuwa  pia Taasisi hiyo hivi sasa inawahaudumia watoto yatima hivyo kuomba jamii ya kitaanzia kuzidi kuwaunga Mkono katika harakati hizo kwa kutoa michango yao ili kuwawezesha kuwafikia watu wengi zaidi

 

Akizungumza katika Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow ameitaka jamii ya Kiislam kujitolea katika mambo ya kher ikiwemo kuwaanda watoto wao katika suala hilo la kutoa sadaka

 

Aidha viongozi   wa Jumuiya hiyo ya Firdaus wamesema kuwa zaid ya shilingi milion mia mbili zimetumika katika ujenzi huo uliohusisha msikiti, chumba Cha kuoshea maiti pamoja na ukarabati wa madrasa katika eneo hilo la msakangoto.

 

Katika risala ya shukran kwa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa msikiti huo utaondosha changamoto ya sehemu nzuri ya kufanyiwa ibada.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...