Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwasilisha taarifa ya makadirio na matumizi kwa mwaka 2021/22 ya Wizara hiyo kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bungeni, Dodoma. Anayefuatilia wasilisho hilo aliyeketi katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Andrea Mathew na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso akichangia hoja baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kushoto aliyeketi) kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/22 ya Wizara hiyo kwa wajumbe wa Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo A. Mathew na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (wanaomsikiliza) wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 Bungeni, Dodoma

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew (wa kwanza kulia) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula mara baada ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni, Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango Malecela na mjumbe wa Kamati hiyo, Ally Jumbe wakipitia taarifa ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 baada ya kuwasilisha kwenye Kamati hiyo Bungeni, Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Masache Kasaka akichangia hoja baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 kwenye kikao kilichofanyika Bungeni, Dodoma


Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2021/22 kwenye kikao kilichofanyika Bungeni, Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...