******************************************
13,march
KAMATI ya Bunge ya
Kudumu Utawala na Serikali za Mitaa imeridhishwa na ukarabati wa shule
kongwe ya wavulana ya Kibaha,pamoja na mfumo wa malipo kwenye hospitali
ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi.
Hayo yalisemwa mjini
Kibaha na Humphrey Polepole akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo
ilipotembelea Shirika la Elimu Kibaha (KEC) kuangalia miradi
inayotekelezwa na serikali ambayo ni ya shule na hospitali ambazo ziko
chini ya shirika hilo.
Polepole alisema
,shule hiyo ilipewa zaidi ya sh.bilioni moja ambazo zimetumika vizuri na
kuonyesha mwonekano mzuri wa shule hiyo kongwe.
“Tumeridhishwa na
ukarabati uliofanyika kwa shule hii ambayo baadhi ya viongozi mbalimbali
wa serikali wamesomea hapa na hii itaifanya elimu kuboreka,” alisema
Polepole.
Aidha alisema kwenye
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi mfumo wanaoutumia wa malipo ya
serikali umeboresha kuongeza mapato na kuboresha mapato.
“Hata hivyo naomba
serikali iendelee na maboresho ya mfumo wa malipo hayo ili kuondokana
malipo ya fedha taslimu na badala yake uwe wa kieletroniki moja kwa moja
bila ya changamoto zilizopo sasa,” alisema Polepole.
Naye Naibu Waziri wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) David Silinde alisema
kuwa serikali imeweka mpango mkubwa wa wananchi wote kuwa na bima ya
afya na kuepukana na malipo ya fedha taslimu.
Awali mkuu wa mkoa wa
Pwani mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa serikali ilitoa kiasi cha
shilingi bilioni 4.7 kwa shule tano kongwe ikiwemo Kibaha pia Ruvu
sekondari milioni zaidi ya 900, Minaki milioni 500, Bagamoyo zaidi ya
milioni 900, Kibiti bilioni 1 ambapo pamoja na fedha za elimu bure mkoa
umepata bilioni 42.9.
Akizungumzia mfumo wa
malipo kwenye hospitali ya Tumbi ,Ndikilo alieleza, mapato yalikuwa
300,000 hadi sasa milioni tatu kwa siku.
Hospitali hiyo ina vitanda 250 na inapokea wagonjwa kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...