Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiangalia shughuli za ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme zikiendelea baada ya kufanya ziara kutembelea mradi wa Julius Nyerere.



Eneo la mradi.
Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza maelezo kutoka Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi ambapo ameelezea hatua kwa hatua shughuli za ujenzi zinavyoendelea.

kazi ikiendelea.
Meneja Uhusiano Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) Johari Kachwamba akizungumzia ziara ya wahariri na faida zake baada ya kuona shughuli za ujenzi katika mradi wa Julius Nyerere.


Mmoja wa mafundi akiendelea na kazi kwenye eneo hilo la mradi wa Julius Nyerere.
Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) Lutenganya Kamugenyi akionesha mchoro kuhusu ujenzi wa bwawa la kufua umeme megawati 2115 baada ya wahariri kufanya ziara ya kutembelea eneo hilo  mradi .


Mradi wa Julius Nyerere linavyoonekana ambapo shuguli mbalimbali za ujenzi zikiendelea.
Kazi ikiendelea.


Baadhi ya wahariri wakielekea eneo ambalo maji ya mto Rufiji yakiendelea kupita wakati shughuli za ujenzi zikiendelea katika eneo hilo la mradi.


 Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Rufiji

SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) limeamua kuwapeleka wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ili kujionea shughuli za ujenzi wa Mradi wa Julius Nyerere zinavyoendelea huku wakielezwa mradi huo unatarajiwa kukamilika Juni mwaka 2022.

Katika kuhakikisha wahariri hao wanauelewa vema mradi huo wa kufua umeme ambao ni mkubwa na wa kihistoria katika nchi yetu, wamepata nafasi ya kuoneshwa maeneo mbalimbali na shughuli zinavyoendelea, ambapo baada ya ziara hiyo watakuwa na uelewa mpana na kutoa taarifa sahihi kwa umma kuhusu mradi huo utakaozalisha megawati 2115 na kuifanya nchi sio tu kuwa na umeme wa kutosha bali itakuwa na uwezo wa kuuza kwa nchi jirani.

Meneja Uhusiano TANESCO Johari Kachwamba amefafanua wakati wa ziara hiyo kuwa, Shirika hilo kwa sasa linaendelea na kutekeleza shughuli mbalimbali za miradi ya umeme kwa kuleta maendeleo kwa wananchi , na watu muhimu ambao wanaweza kufkisha taarifa kwa wananchi ni wanahabari.

"Mara kadha tumekuwa tukiwaleta wanahabari kuja kwenye mradi huu kwa ajili ya kuelezea hatua mbalimbali za ujenzi zinavyoendelea, lakini safari hii tumeamua  kuwaleta wahariri wa habari ambao muda mwingi wako kwenye vyumba vya habari wakitekeleza majukumu yao.

"TANESCO tumeona ni vema wakapata fursa ya kuhafahamu kwa kina kuhusu mradi wa Julius Nyerere ambapo hata akiwa anahariri habari inayohusu huu mradi anakuwa na picha kamili ya nini kinaendelea, hivyo tumewaleta ili waone.

"Natunaposema mradi mkubwa ndani yake kuna miradi mingine 10 ambayo inatekelezwa, wahariri wameona sehemu ambayo umeme utakuwa unazalishwa, wameona jinsi ambavyo utakuwa unapita katika hatua mbalimbali, hivyo watakuwa na tafsiri rahisi ya kuelezea wananchi jinsi gani ambavyo Serikali inavyotumia kodi za wananchi kuleta maendeleo.

"Hata tunaposema  uwekezaji wa Serikali ni mkubwa Mhariri atakuwa anajua unazungumzia kitu gani au anahariri kuhusu kitu gani, kwa hiyo mwananchi anapata taarifa za uhakika kuhusu mradi huo,"amesisitiza Kachwamba huku akisisitiza ni matumaini ya TANESCO baada ya wahariri kupata nafasi ya kutembelea mradi huo na kuona kila kinachoendelea, ile haki ya mwananchi kupata taarifa sahihi inakwenda kutekelezeka.

WALICHOKISEMA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI

Baada ya wahariri kupata maelezo kutoka kwa watalaamu mbalimbali wanaosimamia na kutekeleza mradi huo kutoka TANESCO ambao ndio wasimamizi wa kuu wa mradi huo kwa niaba ya Serikali, wahariri wametoa maoni yao na wengi wao wamefurahishwa na uwekezaji mkubwa ambao Serikali umeufanya katika mradi huo.

Mhariri kutoka gazeti la Habari Leo, Mgaya Kingoma amesema baada ya wa hariri kutembelea mradi huo jukumu kubwa lililopo mbele yao ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kuhusu mradi huo ambao una manufaa makubwa kwao baada ya kukamilika Juni mwaka 2022.

"Mradi huu utakapokamilika sio tu unakwenda kuongeza nishati ya umeme, bali pia unakwenda kukuza utalii , utasaidia kwenye kilimo cha umwagiliaji na utunzajiwa mazingira, lakini pia umesaidia watanzania wengi kupata ajira.

"Kwa hiyo sisi wahariri ni jukumu letu kuhakikisha tunawaeleza watanzania huu mradi ni wa kwao, walioko karibu wanatakiwa kushirikiana na Serikali katika kuutunza na kuwa endelevu na kwa wale wengine kuiunga mkono Serikali yao katika kuhakikisha miradi hii ya maendeleo inafanikiwa ili Watanzania waendelee kufurahisha maisha bora.

Kwa upande wake Mhariri kutoka gazeti la Mwananchi Lilian Timbuka kwanza ameelezea kufurahishwa na hatua ambazo Serikali inazichukua katika kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wenye kutosheleza mahitaji lakini kuhusu jukumu la wahariri baada ya kutembelea mradi huo ni kwamba wanawajibu mkubwa kuutangaza huo mradi wa Julius Nyerere.

"Tumeshaona miradi mingi inayotekelezwa na TANESCO lakini kwa mradi huu ni wa mfano na wa kimkakati.Baadhi ya wananchi hawajui nini ambacho kinaendelea kwenye mradi huu, hivyo sisi wahariri na vyombo vyetu vya habari tunayo haki na wajibu wa kuutarifu umma nini kinaendelea kwenye mto Rufiji.

"Kabla ya mradi huu waliyapata mengi kutoka nje ambayo yanakatisha tamaa lakini tumefika hapa tumejionea wenyewe mazingira yalivyo , ujenzi unavyoendelea na wamtuhakikishia kwamba mwakani Juni hili bwawa litakuwa tayari, hivyo tunaimani kabisa ile kauli mbiu ya Serikali ya viwanda ambayo Rais wetu amekuwa akiizungumzia sasa inakwenda kuwadia,"amesema Timbuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...