Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Advocate Stephen Byabato ametekelea ahadi yake ya kusaidia Watoto ishirini Vifaa vya Shule kila Kata kwa Kata 14 Jimboni, hadi aliyoitoa siku Chache baada ya kupata wadhifa wa Naibu Waziri wa Nishati.

Watoto hao 280 wanaoishi katika familia Duni na wale ambao walishaondokewa na Wazazi wao (Yatima), wamepatiwa msaada huo wa sare za Shule, madaftali na kalamu vikitolewa na Diwani wa Kata Hamugembe Muhaji Kachwamba ili kupunguza makali ya gharama za Elimu.

Akizungumza kwa hisia wakati wa shukrani kwa Niaba ya wenzake mbele ya ugeni wa Mhe. Mbunge Byabato,  Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Shaniat Amir ameshukuru Mhe. Byabato kwa wazo lake la kuwakumbuka Watoto hao na kuwachangia kidogo hicho.

Mhe Stephen Amesema sare hizi zimetolewa kwa wanaostahili kupewa mahitaji hayo ikiwa Ni Mchakato iliyofanywa na Madiwani wa kata husika kwa Kushirikiana na TASAF pamoja na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Bukoba, na kuongeza kuwa huu ni mwanzo wa kutekeleza shughuli zilizopo kwenye Ilani na ambazo hazipo katika Ilani. 

Picha ya Pamoja Mhe. Mbunge Byabato, Diwani Muhaji Kachwamba, Viongozi, Wazazi na Wanafunzi
Muonekano wa Watoto wa Kata Hamugembe wakiwa wamependeza ndani ya sare zao Mpya baada ya kukabidhiwa sare hizo na Mbunge Byabato.

Mbunge Adv. Stephen Byabato akikabidhi sare za shule kwa moja kati ya Watoto wanaoishi Kata Hamugembe katika Mazingira magumu, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa.

 Mbunge Adv. Stephen Byabato akikabidhi Daftali na kalamu kwa moja kati ya Watoto wanaoishi Kata Hamugembe katika Mazingira magumu, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa.

Sare na kalamu na Daftali zilizotolewa na Mhe. Mbunge Jimbo la Bukoba Mjini Advocate Byabato pamoja na Diwani Kata Hamugembe Muhaji Kachwamba kuwasaidia Watoto wanaoishi Mazingira magumu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...