CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimeeleza kuguswa na kifo cha aliyekuwa Rais Dk. John Magufuli na kuwataka watanzania kusimama pamoja ili kuyaenzi mema aliyoyafanya.

Pia kimesema kina imani na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuliongoza taifa kwani jina lake pekee limejipambanua kuwa ni mleta suluhu.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia , wakati alipofika kutia saini kitabu cha maombolezo ya Hayati Rais Dk. Magufuli, katika Ukumbi wa Karmjee.

“Tukitumia hekima zetu vizuri tukawa na utulivu wa fikra tukasikilizana tutamsaidia sana Rais aliyepo sasa wa sita wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniua, mama yetu Samia Suluihu Hasan,”alisema Mbatia.

Aliongeza; “Jina lake ni suluhu na na ataleta suluhu kwa taifa ili tuunganishe yale yote yaliyofanyika tangu enzi za nyerere ambaye alifanya mambo mengi ndani ya nchi yetu hata sasa,”.

Mbatia alisema ameguswa na kifo cha Dk. Magufuli na kwamba yako mambo ambayo alijaliwa na Mwenyezi Mungu, akaumia akayanzisha akiwa zawadi kwa watanzania kuweza kuyafanya ili kuifanya Tanzania kuwa salama na kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuishi.

“Ni seme tu buriani Rais Dk. Magufuli, sisi wote hapa duniani tunapita. Kifo ni mtihani na nifumbo la uumbaji kwamba binadamu aliyezaliwa kuna kufariki pia,”alibainisha.

Alisema kwakuwa Hayati Dk. Magufuli alimtumaini na alimwamini mwenyezi Mungu anaamini yale yote mema aliyoyatamani na aliyoyaanzisha basi Mwenyezi Mungu ataweka mkono wake ili kasi hiyo iweze kukamilika.

“Kwa kuwa kwenye wimbo wetu wa taifa tunaamini uwepo wa mwenyezi Mungu na ndiyo maana tunaimba Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania na ndani ya wimbo wetu wa taifa tuna nguzo kuu tatu, nguzo ya hekima nguzo umoja na amani hivyo tunatakiwa kuwa na utilovu wa fikra,”alibainisha.

Alisema yote yatawezekana eendapo watanzania wakiwa na umoja wa kitaifa.

“Tanzania ikiwa ni sehemu ya nchi za maziwa makuu na katiba Bara la Afrika tunahistoria ya kuwa kituo cha ukombozi wa kusini mwa afrika.

Na kanuni ya Mwalimu Nyerere ya aliyoanzisha ya kwamba binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja, basi tuwe ndugu wa pamoja, msiba huu utuunganishe pamoja,”alieleza mwanasiasa huyo.

Alisema siyo rahisi kukubari msiba lakini ufike wakati watanzania wakubari kuwa umetokea .

Mbatia aliambatana na Katibu Mkuu wa NCCR-Magezi , Martha Chiombe.

Hayati Rais Dk. Magufuli alifariki Machi 17 mwaka huu katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya moyo na anazikwa leo, Chato mkoani Geita.

MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, akitia saini kitabu cha maombolezo cha Hayati Rais Dk. MJohn Magufuli, katika Ukumbi wa Karmjee, Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...