Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametangaza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) baada ya kubainika kuwepo kubadhilifu wa fedha za Serikali zaidi ya Bilioni 3.6.

Akizungumza wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019-2020, Rais Samia amesema Mkurugenzi huyo atasimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa upotevu huo wa Fedha hizo za Serikali.

Pia Rais Samia ameziagiza TAKUKURU na CAG kuangalia Mifumo ya ukusanyaji wa Mapato, ameagiza kuwepo kwa Mifumo maalum ambayo itatumika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato hayo ya Serikali.

Hata hivyo, Rais Samia amegiza Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuangalia zaidi urudishaji wa fedha za Serikali sio tu kuchukua tu fedha hizo kufanyia miradi mbalimbali.

Amewaagiza CAG kusimamia Mashirika na Taasisi zisizofanya vizuri kwa kuhakikisha Ripoti zinazotolewa na kuwasilishwa kuwa za wazi zaidi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...