WAKATI bado tunaomboleza msiba mzito wa Taifa wa kuondokewa na Mpendwa wetu, Aliyekuwa Rais wa Taifa letu la Tanzania, Mpenda Amani, Mpenda watu wake hususani wale wenye hadhi ya chini na kipato kidogo, Mpenda Maendeleo, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Kaka Peter Msechu naomba niongee na wewe kitu katika Tasnia yako ya Muziki...

Kiukweli baada ya kutangazwa Kifo cha Hayati Dkt. Magufuli Machi 17, 2021 na Aliyekuwa Makamu wa Rais kipindi hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, Wasanii wengi nchini walijitokeza kutunga tungo (Nyimbo) mbalimbali kumuenzi Mpendwa wetu aliyetangulia mbele ya haki.

Tumeona tungo nyingi zilizojaa wasifu wakumuenzi Hayati Dkt Magufuli, tungo hizo kutoka kwa Wasanii hao wa Tanzania na Vikundi mbalimbali vya Muziki ziliwavutia watu wengi kutokana na kubeba ujumbe wa kweli kwa Taifa letu. Tumeona vikundi kama Tanzania One Theatre (TOT), Vikundi kutoka Makanisa mbalimbali nchini na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya kama kina Diamond Platnumz, Harmonize, Alikiba, Rayvann, na wengine wengi.

Lakini kwa Msanii Peter Msechu tungo zake zilivutia wengi kwa kiasi kikubwa kutokana na kubeba ujumbe wa kweli na zenye kumuenzi Mpendwa wa Taifa la Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, yote ni kutokana na Maendeleo na yale yote yaliyofanyika chini ya uongozi wake kabla ya kufariki dunia.

Tazama Kibao cha TUTAONANA MAGUFULI, ni Kibao kilichotulia ambacho unaweza kusikiliza wakati wowote bila kuchoka kutokana na tungo zake ndani yake, Vyombo mbalimbali vya Habari nchini vilionekana kupiga vibao vya Peter Msechu mara kwa mara sambamba na Nyimbo nyingine nyingi za Maombolezo za Wasanii wetu wa Tanzania.

Sikiliza Kibao UMETUACHA IMARA ni kibao  kilichobeba Ujumbe wa kumuenzi Hayati Magufuli kwa yale yote aliyoyafanya katika Taifa la Tanzania katika kipindi chake chote alichokuwa madarakani kabla ya umauti kumkuta, tazama na sikiliza ‘Melody’, ‘Beats’ kwa wale wanaojua muziki kwa hakika utafurahia kilichofanywa na Peter Msechu. Hongera Kaka!.

“Umetuacha imara, Tanzania Salama
Magufuli lala Salama, Mwenda umeumaliza

Umetuacha imara, Tanzania salama
Magufuli lala, Mungu akulaze pema peponi.
Nguzo yetu imara imeanguka inauma, Shujaa wetu shupavu ona amelala...
Amefanya makubwa, yakuigwa ya mfano.

Magu tunakulilia, Twatamani urudi kidogo
Mungu kwa nini umeruhusu, Mwamba wetu aende
Tumebaki na ukiwa, nafsi zimejaa giza, Magufuli lala Salama, tutaonana baadae sote njia yetu moja, tangulia twaja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kusema ukweli, Msechu nyimbo zake hizi mbili zimegusa mioyo ya watu mno. Barikiwa sana, barikiwa wasanii wote mliomuimbia jemedari wetu. Apumzike kwa amani JPM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...