Na Mwaandishi Wetu Mtwara
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelesius Byakanwa ametoa siku saba kwa wafanyabiashara wa soko la sabasaba kuhamia soko la Chuno ambalo ni soko la kisasa lililojengwa na serikali kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
Byakanwa ametoa rai wakati wa ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Ali Maulidi ambaye alitembelea soko hilo kama sehemu ya ziara yake ya kukagua miradi ya kimkakati ya serikali katika Mkoa wa Mtwara.
“kwa wale ambao mnafanyabiashara sabasaba kwa wiki moja, mpanaswa kuhamia hapa Chuno, baada ya tarehe 17, Mkurungezi wa manispaa kutumia mgambo, sitakai kukuta meza, sitaki kukuta biashara yoyote inafanyika sabasaba,” amesema Byakanwa.
Soko hilo ambalo ujenzi wake uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3 lilifunguliwa mwaka jana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba kutakiwa kuhamia kwenye soko hilo.
Pia alimtaka Mkurungezi wa manispaa kutoa ruti ya daladala kwa ajili ya kwenda soko la Chuno ili kurahisisha usafiri kwa wateja wa bidhaa za wafanyabiashira soko la Chuno.
Byakanwa amesema kuanzia tarehe 17 hakutakuwa na biashara yoyote na huku akiahidi kufanya ufuatiliaji kuhakikisha biashara hazifanyiki sabasaba.
“Mgeni rasmi nakuhakikishia kwa nguvu zangu nilizonazo, kwa uwezo wangu alionipa mwenye Mungu, nitasimamia hili na kuhakikisha haki za akina mama zinapatikana,” amesema.
Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo baada ya akina mama wafanyabishara wa soko la Chuno kutaka serikali ya mkoa kutoa tamko ili wafanyabiashara waliopo soko la Sabasaba kuhamia soko la Chuno na kuondoa sintofaham kwa wateja na wafanyabiashara kwenye soko la Chuno.
Pale sababsaba ambapo wanatumia mipangoo miji, sio siko, ili ni paking na waliruhusu itumika kwa mda kwa sababu kipidi kile hapakuwa na soko , kwa sasa hivi lijenhwangwa soko na kwa kuwa tumejenga soko hakuna sababu ya kutumia maegesho ya magari sabasaba.
Akizungumza na wafanyabiashara akina mama waliojitokeza kulalamikia baadhi ya wafanyabiashara kutokuhama sabasaba, Spika huyo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Maulidi amewaasa wafanyabishara ambao bado wapo katika soko la sabasaba kutii agizo la Mkuu wa Mkoa na kuhama ili kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza wakati wakilazimika kutoka kwa nguvu.
Amesema serikali ya CCM ni sikivu na kwamba itahakikisha inaweka huduma zote zinazohitajika katika soko hilo jipya zikiwemo huduma za usafiri kwenda kwenye soko la Chuno.
“La muhim ni kwamba watu wahame sabasba kuepush usumbufu , mtu aanze kuhama mwenyesi zisitumike nguvu kuhamishwa,” amesema.
Mapema wakitoa malalamiko yao mbele ya ujumbe ukiongozwa na Spika Maulidi, akina mama wafanyabiashara wa soko la Chuno walisema biashara katika soko la Chuno zimedorora kutokana na ukosefu wa wateja katika soko hilo.
Tatu Abdallah mfanyabiashara wa soko la Chuno amesema toka wahamie soko hilo jipya wameshindwa kufanya biashara zao kwa ufanisi kutoka na kukosekana kwa wateja huku akitaka serikali itoe tamko ili wafanyabiashara walioko sabasaba wahamie soko jipya.
“Toka tuhamie hapa biashara zetu ni kama zimekufa, tunataka serikali itoe tamko tujue soko la jumla liko wapi kama ni sabasaba basi turudi sabasaba na kama ni hapa Chuno, wale wafanyabiasha walioko sabasaba waje hapa chuno,” amesema na kuongeza kuwa wafanyabiashara wa soko la chuno wamekuwa wanakosa wateja kutokana na kwamba bado soko la sabasaba lipo licha ya kuwa na soko jipya.


Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Zuberi Ali Maulidi akipata maelezo kutoka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa kuhusu mradi Soko jipya la Chuno ambalo limejengwa na serikali ya thamani ya shilingi bilioni 5.3.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...