Na Woinde Shizza ,Michuzi - Tv 

SERIKALI  imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu ya elimu na miradi mingine ya  maendeleo katika halmashauri ya Jiji la Arusha kwani  imetekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kulingana na  fedha zilizotolewa kwa miradi husika .

Mkuu wa Wilaya ya Arusha  Kenan Kihongosi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Arusha kwenye mkutano wa robo ya Pili wa Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa.  

Alisema kuwa anajivunia kuona fedha za miradi zilizotolewa na Serikali ya   Dk.John Pombe Magufuli  zimetumika ipasavyo na miradi imekamilika kwa asilimia 95 kwamba kukamilika huko  kumewezesha  wanafunzi kujiunga kidato cha kwanza bila kikwazo.

Aliendelea kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk. John Pima kwa kusimamia vyema fedha za Serikali na kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati. 

Pamoja na mambo mengine alisema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kwa ushirikiano wa madiwani na wataalam na kudai kuwa Serikali inajivunia uongozi huo. 

Awali Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe alipongeza jitihada za Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa madarasa mwaka 2020 na kwamba Kiongozi huyo  ni mfano wa kuigwa. 

Iranqhe alisema kuwa nia ya Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha nikuwaletea Wananchi Maendeleo na kudai kuwa Arusha itakuwa mji wa mfano kwa kuwaletea wananchi maendeleo. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...