MAHAKAMA Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi,  imemuhukumu blogger Shamimu Mwasha (41), na mume wake Abdul Nsembo, maarufu kama Abdulkandida (45)  kutumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hukumu hiyo imetolewa leo Machi 31, 2021 na Jaji Elieza Luvanda baada yaa kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi sita wa upande wa mashtaka. 

Shamimu anayemiliki Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, walikuwa  wanakabiliwa na 

mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 232.70, kosa wanalodaiwa kulitenda Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es. Salaam.

Shamim Mwasha wakiwa na Mumewe, walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...