Na Woinde Shizza , Michuzi Tv - ARUSHA

Mwenyekiti wa taifa wa chama cha wafayabiashara wa madini Tanzania Sammy Mollel ameeleza kuwa wamepokea kwa masikitiko makubwa na simanzi taarifa za kifo cha hayati Rais Dkt John Magufuli kwani alikuwa jemedari wao katika kusimamia biashara ya madini.

Mollel aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa hawakuamini walipopata taarifa za awali lakini baada ya makamu wa Rais mama Samia Suluhu kutangaza ndipo wakagundua kuwa ni kweli.

“Kifo cha hayati Rais Dkt Magufuli kimetugusa sana wafanyabiashara wa madini jitihada na maono yake yalipandisha makusanyo ya tozo za madini kutoka millioni 160 kwa mwaka hadi kufikia billioni 2,”Alisema Mollel.

Alisema wameona juhudi zake binafsi za kujengwa ukuta Mererani ambapo mpaka sasa wameona faida kubwa sana za ukuta huo ikiwemo kulinda usalama wao wanapokuwa katika kazi zao tofauti ma awali, uzalishaji kuongezeka pamoja tozo za serikali kukusaywa kwa kiasi kikubwa.

“Ameifanikisha sana sekta ya madini kwa kuelekeza masoko ya madini yajengwe kila mkoa wenye shughuli za uchimbaji madini, tulimweleza kero zetu kuhisiana tozo sumbufu, alizipokea na kutoa maelekezo kwa Bunge kurekebisha ambayo ilikuwa ni tozo ya ongezeko la thamani, VAT na tozo ya zuio na kushuka kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 5,” Alieleza.

Alifafanua kuwa walimpenda sana lakini Mungu alimpenda zaidi na kama Tamida wanawasihi watanzania kuwa na subira kipindi hiki cha maombolezo na kuyaezi yale yote aliyowaachia kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kuigia katika uchumi wa juu.

“Kwa sababu yake leo Tanzania tuna heshima kubwa sana duniani kwa kuingia uchumi wa kati na uchumi wa viwanda na sisi tunaahidi tutamuenzi kwa kuongeza dhamani ya madini na kufika mbali zaidi kama alivyotuazishia,”Alieleza.

Kwa upande wake bilionea wa madini aina ya ruby kutoka wilayani Longido Gabriel Sendeu Laizer alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo cha Rais Magufuli kwani alikuwa akiwathamini wachimbaji wadogo wa madini haswa wazawa wa kitanzania.

Alisema kuwa Rais Magufuli aliweza kuwapa haki zote za uchimbaji wa madini pamoja na umiliki wa madini kwa kuwawezesha pamoja na kuwa na nguvu zao wenyewe ambapo pia hakujali kwamba wachimbaji wazawa wataweza kuchimba au awawezi kuchimba .

Alisema kuwa kutokana na Magufuli kuwathamini na kuwapa fursa watanzania wameweza kuchimba madini na kujipatia kipato.

"Amewezesha migodi ambayo ilikuwa imesimama kutokana na kuachwa na wazungu kuchukuwa na wazawa , kazi zinaendelea na ndio maana unaona hata mapato yanayotokana na madini yameongezeka kuliko wakati mungine wowote ule" alisema Sendeu.

Alimpongeza Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuongoza nchi ya Tanzania ,na kukwambia kuwa wanamtakia mafanikio mema katika kazi zake za kuletea nchi maendeleo

Alisema kuwa wanaamini kabisa Rais ata endeleza yale yote mema ambayo hayati Magufuli ameyafanya ,ikiwemo miradi mbalimbali waliyoiacha .

300 mchimbaji wa madini aina ya Ruby ,bilionea Gabriel Sendeu Laizer akionyesha moja ya mawe aliyoyapa kipindi cha Rais Magufuli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...